• KILIMO BORA CHA ZAO LA GILIGILANI

    KILIMO BORA CHA ZAO LA GILIGILANI
    Giligilani ni zao ambalo huchukua kati ya siku 35 hadi 40 tangu kupandwa hadi inapokuwa tayari kwa kuvuna majani yake;
    Kwa uvunaji wa mbegu huchukua hadi siku 45 tangu kupanda hadi zinapokuwa tayari.


     
    MAHITAJI YA MMEA
    • Giligilani huitaji mwanga wa jua la moja kwa moja kiasi cha masaa 6 kwa uchache ila inapendekezwa zaidi masaa 8 au zaidi kwa ukuaji mzuri wa mmea na kuwa na majani yenye harufu nzuri
    • Giligilani huweza kuwa na ladha nzuri zaidi inapopata jua la kutosheleza. Mwanga mkali wajua husaidia kutengeneza majani yenye harufu nzuri zaidi.
    • Unapo chagua eneo la kupanda giligilani angalia udongo ambao unaweza kupitisha maji vizuri. Unaweza kuweka mbolea ya asili (organic matters) ili kuwezesha udongo wako uwe na drainage nzuri.
    • Giligilani tofauti na mimea mingine hua haihitaji matumizi makubwa ya mbolea kuwekwa kwenye udongo kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuathiri ladha ya majani ya mmea huu

    MAANDALZI YA UDONGO
    • Giligilani hustawi vizuri kwenye udongo wenye pH 6.0 hadi 8.0 ingawa hufanya vizuri zaidi kwenye udongo wa size ya kati yaani pH 7.0
    • Kwa matokeo mazuri hakikisha unatifua vizuri udogo wako na kuuchanganya vyema na mbolea ya asili
     
    UCHAGUZI WA MBEGU BORA
    Giliglani zipo mbegu za aina mbili, zipo zinazolimwa kwa ajili ya kuvuna mbegu, pia zipo zinazolimwa kwa ajili ya kuvuna majani.
    • Unapotaka kulima giligilani kwa ajili ya kuvuna majani, unashauriwa kutumia mbegu ambazo ni maalum kwa ajil hiyo ambazo zenyewe huchelewa kutoa mbegu na hutoa mbegu chache.
    • Kama utapanda kwa ajili ya kuvuna mbegu, basi zipo mbegu maalum kwa ajili hiyo ambazo zenyewe hutoa tunda za mbegu mapema zaidi na hutoa mbegu nyingi

    UOTESHAJI WA MBEGU
    Kwakuwa giligilani ni mmea ambao huwa una sifa ya kuwa na mzizi mrefu unakwenda chini zadi unashauriwa kupandikiza mbegu shambani moja kwa moja ila hata ukianzia kwenye kitalu utaota pia.
    Giligilani huoteshwa kwa spacing inch 6 kutoka mmea mmoja hadi mwengine na inch 12 kutoka mstari mmoja hadi mwengine

    UOTESHAJI KWA NJIA YA KITALU
    • Hakikisha upatikanaji wa mwanga wa kutosha kati ya saa 14 hadi 16 kwa siku
    • Tumia vyombo maalum vitakavyo kuwezesha kuhamishia mima shambani bila kusumbua mizizi ya mmea
    • Waweza weka virutubisho vya alfalfa vitasaidia mimea yako kukuwa mapema.
    • Panda mbegu zako ¼ hadi ½ inch kina.
    • Usishindilie udongo uwe unamwagilia maji ya kutosha hadi mbegu zitakapo anza kuota

    KUHAMISHIA MICHE SHAMBANI
    • Ikifikia urefu wa inch 2 hadi 3 mimea yako itakuwa tayari kuhamishiwa shambani.
    • Kuhamisha miche shambani kunapaswa kufanyika kwa utaratibu wa kuuzoesha mmea taratibu kuzoea mazingira ya nje.
    • Peleka mimea yako mazingira ya nje kwamuda mchache kwa kuanzia na kadri siku zinavyo sogea ongeza muda zaidi (Fanya zoezi hilo kwa kati ya siku 7 hadi 10)
    • Hamisha mmea na udongo wake ili kuepuka kusumbua mizizi

    UOTESHAJI KWA KUPANDIKIZA MOJA KWA MOJA SHAMBANI
    • Panda mimea yako kwa mistari miwili kwa utengano wa inch 12 kutoka mstari mmoja hadi mwengine.
    • Panda mbegu zako kwa kina cha ¼ hadi ½ inch na kwa nafasi ya inchi 6 kutoka mmea hadi mmea.
    • Shindilia udungo kidogo sana kisha mwagilia maji kiasi.
    • Kama unataka kuwa na mavuno endelevu waweza kupanda kila baada ya siku 10 hadi 14
    UMWAGILIAJI WA MAJI
    • Mbegu za giligilani huhitaji hali ua unyevu unyevu kwenye udongo.
    • Kama udongo wako ni kichanga utahitajika kufanya umwagiliaji mara kwa mara na sio mara moja kwa wingi, pia kutumia matandazo kutakusaidia kuhifadhi unyevu unyevu.
    • Unashauriwa kutumia drip irrigation kwa matokeo bora zaidi

    UVUNAJI WA GILIGILANI
    • Giligilani huanza kuvunwa inapofikia urefu kiasi cha inch 6, uvunaji hufanya kwa kuchuma miche ya pembeni na kuacha mche mkuu wa kati. Uvunaji wa mara kwa mara husaidia kuchelewesha giligilani kutoa mbegu mapema
    • Ni bora zaidi kuvuna giligilani wakati ambapo uko tayari kuitumia ama kweny salad au vyakula vingine.

    UHIFADHI
    • Giligilani ikisha vunywa inatakiwa kuwekwa kwenye chombo chenye maji na kuhifadhiwa kwenye jokofu ili isinyauke na kupoteza ubora wake
    • Giligilani huwa haihifadhiwa kwa kukausha kwana kwa kufanya hivyo hupoteza kabisa ladha yake

    NJIA ZA KUFANYA ILI UVUNE MAJANI KWA MUDA MREFU
    -Chagua mbegu ambazo hazitoi maua mapema
    -Panda mbegu kwa kupishana kati ya week hadi week mbili kujihakikishia mavuno endelevu
    -Vuna mara kwa mara majani, uvunaji wa mara kwa mara huchelewesha mmea kutoa maua
    -Panda mimea karibu karibu sana kuhakikisha jua kali halfikii udongo kwani joto kali la udongo ndilo hupelekea mmea kutoa maua mapema au weka matandazo juu ya udongo.

    UVUNAJI NA UHIFADHI WA MBEGU
    • Kama utaiacha mimea yako kwa ajili ya uvunaji wa mbegu, kata vikonyo vya maua, bakisha kiasi cha inch 3, viweke kwa pamoja vikonyo hivyo ulivyokata, vifunge kwa pamoja kwa kutumia kamba au mpira.
    • Ning’iniza vikonyo hivyo vya maua juu chini kwenye mfuko kuhakikisha mbegu hazimwagiki kasha tundika mfuko huo ambao umefungwa vizuri kwenye sehemu kavu na yenye giza
    • Kwenye kipindi cha week moja tingisha mfuko huo na mbegu zitadondokea ndani ya mfuko huo kisha zikusanye na uziweke vizuri kwenye chombo kikavu tayari kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadae ya kupanda tena

    TABIA ZA MMEA
    Giligilani ukishatoa maua ya mbegu ladha ya majani hupotea haraka sana, kukata maua hauwezi kuufanya uendelee kuvuna majani, unashauriwa kuacha maua yaendelee ili uje kuvuna mbegu unazoweza kuzitumia kwa matumizi ya baadae.
    Mmea ukishatoa maua hauwezi kuendelea kutumika tena kwa matumizi ya kuvuna majani.
    Kwenye kipindi cha joto kali seli za mmea huchochea mmea kutoa maua haraka ili kutengeneza kizazi kipya cha mbegu ili zao liendelee kuwepo kabla mme haujafa.

    MIMEA WASHIRIKA WA GILIGILANI
    • Giligilani ina uwezo wa kufukuza wadudu kama vile aphids na buibui.
    • Mazao kama Carrots, cabbage, spinach, pia hufaidika yakipandwa na giligilani
    • Giligilani hufaidika ikipandwa pamoja na mimea jamii ya mikunde, kama vile mbaazi na maharagwe ambayo hufyonza hewa ya nitrogen kutoka angani na kuingiza chini ya udongo

    WADUDU WANAO WEZA KUSHAMBULIA ZAO HILI NA NAMNA YA KUTIBU
    • Leafhoppers ni mdudu ambae anaeneza ugonjwa Aster’s Yellows. Wadudu hawa hijificha chini ya jani la mmea, hufonya maji maji ya mmea kwenye majani na kuingiza bacteria wadogo wadogo, hudhoofisha mmea hali ambayo inaweza kupelekea mmea kufa.
    Tumia dawa za kuuwa wadudu kama vile, neem oil, pyrethrum, au Diatomaceous Earth (DE) zote zimekuwa na matokeo chanya kwenye kupambana na wadudu hawa.
    • Aphids hupatikana chini ya jani la mmea. Hufanya majani ya mmea kuwa njano na kusinyaa au kukauka.Hufyonza maji maji kutoka katika majani ya mmea na kuacha matone yenye hali ya kunata
    Tumia insecticidal soap au Diatomaceous Earth (DE) zimekuwa na matokeo chanya kwenye kukabiliana na tatizo hili.
    • The armyworm (Kiwavi jeshi), Wenyewe hula majani ya mmea, na kudondosha punje ndogondogo za majani chini ya mmea.
     
    MAGONJWA
    • Leaf spots husababishwa na umwagiliaji kwenye majani ya mmea ambapo husababiswa na maji yenye vimelea vya bacteria.
    • Namna ya kukabili tatizo hili ni kutumia drip irrigation lakini pia neem oil and organic copper-based fungicides zinaweza kusaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.
    • Root Knot Nematodes ni ugonjwa unao fanana na minyoo, mara nyingi mimea ambayo haipati maji ya kutosha hupelekea kupata ugonjwa huu. Ugonjwa huu hupelekea mimea kudumaa, kupunguza mavuno na wakati mwengine huua mimea.
    Uonapo ugonjwa hu shambani unashauriwa kuliacha shamba kwa kipindi cha miaka 2 hadi 3. Pia usiruhusu maji kutokea sehemu ambayo imeathiriwa kwenda sehemu ambazo bado hazijaathiriwa
    Giligilani tofauti na mazao mengine mara nyingi halisumbuliwi na magonjwa kabisa. Mara chache sana zao hili hushambuliwa na ukungu ambao husababishwa na wingi wa maji shambani hasa linapooteshwa wakati wa mvua kubwa na wakati wa baridi kali. Hakikisha unamwagilia kwa kiwango cha wastani huku ukiepuka kuotesha wakati wa mvua nyingi na wakati wa baridi kali.

    FAIDA ZA GILIGILANI KWA AFYA YA MLAJI
    • INASAIDI KUONDOA HEAVY METALS KWENYE MWILI
    • HUSHUSHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE DAMU
    • KINGA YA MAGONJWA YA MOYO
    • KINGA DHIDI YA U.T.I
    • KINGA DHIDI YA SUMU ZIPATITIKANAZO KWENYE VYAKULA
    • KINGA DHIDI YA KANSA YA UTUMBO
    • INASAIDIA KUTULIZA MFUMO WA KINGA MWILINI KUTOKANA NA MADHARA YATOKANAYO NA ALLERGE
    • INASAIDIA KUPUNGUZA UZITO
    • INASAIDIA KUYEYUSHA CHOLESTROL
    • INAZUIA BACTERIA KUZALIANA
    • INA IMARISHA MFUMO WA KINGA MWILINI
    • INAZUIA KANSA YA MAPAFU
    • INAONGEZA HAMU YA KULA NA KUSAIDIA MMENG’ENYO WA CHAKULA
    • INASAIDIA KUSAFISHA DAMU
    • INASAIDIA KUIMARISHA MIFUPA

    KWA MAONI NYONGEZA AMA USHAURI TUNAKARIBISHA MAONI YA WADAU WENGINE









    Source: Smart Ideas


    No comments:

    Post a Comment