KILIMO BORA CHA CHOROKO (MUG BEAN)
UTANGULIZI
Choroko ni zao la chakula na zao lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium.Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 800 hadi 1000 kwa ekari.
UDONGO NA HALI YA HEWA IFAAYO.
Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu. Zao hili hufanya vyema zaidi kwenye udongo wenye pH kati ya 6.2 na 7.2.
Choroko ni mimea inayohitaji joto kati ya nyuzi 27 °C hadi 30 °C. Choroko ni zao ambalo linaweza kustahimili joto na ukame.
AINA ZA CHOROKO
Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.
1. CHOROKO ZINAZOTAMBAA-hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.
2. CHOROKO ZINAZOSIMAA=Hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusima kwenda juu.
KIPINDI KIZURI CHA UPANDAJI WA CHOROKO
Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.
NAFASI ZA UPANDAJI WA CHOROKO NA KIASI CHA MBEGU
Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8 )sentimeta
SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.
UMWAGILIAJI
Kama umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji basi mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada ya mbegu kuota kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za kumwagilia zinatosha kwa choroko.
PALIZI
Palilia shamba lako mapema kuzuia magugu.Palizi moja inaweza kutosha.
MAGONJWA YA CHOROKO
1) yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)
Dalili- mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.
Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.
2) Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.
Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).
anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali halisi.
3) LEAF SPOT (Vidoti katika majani)
Dalili-majani yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo katikati yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari ya rangi ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha hasara hadi ya asilimia 58 ya mapato.
Kinga na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea hii na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu (Fungicide) Katika nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom linashambuliwa mara kwa mara na ukungu.
WADUDU
Kuna wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile aphidi,funza wa vitumba,nzi wa maharage.
Wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wdudu mara tu baada ya mimea kuota,dawa kama karate,twigathoate,dimethote na nyinginezo zinaweza kutumika.
URUTUBISHAJI KUONGEZA MAZAO
Tumia booster ya choroko kwenye mimea yako ambayo ina wingi wa (Potassium and phosphorous)
UVUNAJI
Mavuno ni kati ya siku 65-72 tangukupanda ambapo vitawi vya mbegu hubadilika rangi kuwa kahawia au nyeusi na majani hubadilika rangi kuwa yanjano hapo choroko zako zitakuwa tayari kwa kuvunwa
Mara tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe ukichelewa zitapukutikia shambani.
MASUALA MUHIMU KWENYE KILIMO HIKI
• Chagua eneo ambalo udongo hautuamishi maji
• Chagua mbegu bora na chagua mbegu ambazo zina uwezo mkubwa wa kuota na kukabiliana na magonjwa.
• Weka mbolea zinazo kosekana baada ya kufanya vipimo vya udongo
• Chagua mfumo mzuri wa upandaji kwa Misatari: Mistari yenye upana wa kutosha hsaidia kwenye zoezi la upandaji, hurahisisha kukabiliana na magugu na wadudu wanao weza shambulia mimea yako; Mistari ilobananishwa huleza mazao mengi ila hupeleke changamoto kubwa ya magugu na wadudu na magonjwa shambani.
• Fanya ukaguzi mara kwa mara shambani kuangalia magugu ili yakabiliwe mapema
• Weka tahadhari kubwa zaidi kwa magonjwa kuanzia siku ya 28 hadi 35 tangu ulipopanda.
FAIDA ZA CHOROKO KIAFYA
• Hupunguza kiasi cha Cholesterol mwilini na kinga dhidi ya magonjwa ya moyo
• Ina Ina Amino Acid kwa wingi ambayo husaidia kupambana na ukuaji wa kansa mwilini.
• Husaidia uzalishaji wa insulin za kutosha na kuepusha maradhi ya kisukari
• Ni chanzo kikubwa sana cha protein
• Ina imarisha mfumo wa kinga
• Chanzo kizuri sana cha Vitamin B9
• Kinga dhidi ya vitambi na kusaidia kupunguza uzito
• Mmeng’enyo wake ni rahisi zaidi kulinganisha na mimea mengine jamii ya kunde kunde
Source: Smart Ideas
No comments:
Post a Comment