UZALISHAJI WA TIKITIMAJI
Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo
tumia siku 65-90 kutoka kupandwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu
uliyotumia na hali ya hewa ya eneo husika kwani maeneo ya pwani na
yenye joto sana tikitimaji na mazao mengine hukomaa mapema ukilinganisha
na maeneo ya milimani yenye baridi kwa hiyo tunashauri kama unataka
kulima tikitimaji basi tafuta sehemu zenye hali ya hewa nzuri kuendana
na mahitaji yako na soko lako lilivyo
ENEO
Chagua eneo ambalo halina historia ya
kuwa na magonjwa au wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji
yanapatikana kwa urahisi kwa
ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji ,pia eneo lisilo na udongo wenye
chumvi chumvi na unaotuamisha maji soma hapa kujua aina za udongo Namna ya kutambua udongo wenye chumvi na namna ya kuondoa chumvi,Njia za kupima na kutambua aina ya udongo kwenye shamba lako,
tikiti maji linastawi sana katika udongo tifutifu na kichanga lakini
udongo wa mfinyanzi sio mzuri sana kwa tikiti maji kwani husababisha
matunda kuwa na nyufa(cracks)
KUANDA SHAMBA.
Lima shamba lako vizuri kwa kuvunja vunja udongo na pia
andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda juu sentimita 30 ili
kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia maji kutuaama hasa katika
kipindi cha mvua.mfano wa picha kwa uandaaji wa shamba
Nikaribishe kwenye shamba lako nikupe utaalamu namna ya kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo hiki na mazao mengine
MFANO WA MASHAMBA YALIYOLIMWA VIZURI TAYARI KWA KUPANDA |
MAHITAJI YA TIKITIMAJI
Tikiti linakua vizuri katika udongo unaoshika maji vizuri
lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH
5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji. Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la
udongo kiasi cha 18-29 0c. Joto chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu
na ukuaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu
wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi katika udongo wakati wowote wa ukuwaji
na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na
ubora wa matunda.
UPANDAJI
Mbegu/mche wa tikiti maji utapandwa mita 1-2 kati ya mmea na
mmea na uwekwa sentimita 2.5 kwenda chini(shimo la kupandia), na kati ya mstari na mstari iwe mita
2,kwa umbali huu panda mbegu 2 kila shimo.Au weka umbali wa sentimita 50 kwa
mita 2 lakini hapa panda mbegu moja moja. katika hekari moja utahitaji mbegu gramu 500gms-600gms
DOUBLE ROW PLANTING |
SINGLE ROW PLANTING |
Mbegu ya tikitimaji utokeza baada ya siku 5-7.
UTUNZAJI WA MMEA.
a) Mbolea.
Mbolea ya samadi kwa kiasi cha 4-6 tani kwa ekari,ichanganye
na udongo wiki moja kabla ya kupanda,pia mbolea hii unaweza iweka katika kila
shimo siku kadhaa kabla ya kupanda kisha mwagilia ili kupunguza kiasi kikubwa
kitakacho hitajika kuweka katika ekari moja.Kama huna samadi tumia Yaramila winner
au DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo ,hakikisha mbolea na mbegu havigusani.
Wiki mbili baada ya miche yako kutokeza weka mbolea ya
kiwandani -N-P-K (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila shimo,hakikisha
unaichimbia chini na isigusane na mmea.
Weka mbolea yenye Calcium kana Yaramila nitrabo gram 10 kwa
kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na
mazuri.
UMWAGILIAJI
Maji kwa sentimita 1-5 katika udongo
yanatakiwa kwa mvua au umwagiliaji ili kupata tikitimaji zuri,kipindi
cha muhimu sana kwa mahitaji ya
maji kwa tikitimaji ni :kabla ya mche kutokeza ,mwanzo wa kutoa maua na
siku 10
za mwisho kabla ya kuvuna.Maji machache kipindi cha kupanda husababisha
kutoota
kwa mbegu,kipindi cha kuweka maua husababisha
matunda machache kutokeza na matunda kukosa maumbo yake.Siku 10 za
kuelekea
kuvuna husababisha matunda kuwa madogo kama maji ya kutosha
yasipopatikana.Matunda yakielekea kuiva punguza umwagiliaji maana kiasi
kikubwa
cha maji kitasababisha kiasi kidogo cha sukari kutengenezwa na kupasuka
kwa
matunda, pia kumbuka kweka mfumo wa utoaji maji shambani yaani drainage
sytem(nitakuonyesha zaidi nikifika shambani kwako) hii itasaidia kuondoa
chumvi na kuhakikisha mazao yanastawi vizuri
Angalizo:
Usimwagilie jion sana hii itasababisha kukua kwa magonjwa
kwa sababu ya kuacha majani ya mmea yakiwa na unyevunyevu .Pia angalia wakati
mzuri wa uchavushaji /wakati ambao nyuki
wanakuwepo shambani mwako hivyo jitahidi kumwagilia mda ambao hautawasumbua
nyuki.
Matandazo.
Ni muhimu kutumia matandazo katika shamba lako ili kusaidia
kutunza unyevunyevu katika udongo na matandazo haya baadaye yakioza uongeza rutuba
katika udongo na pia kusaidia kuzuia kumea kwa magugu na husaidia tunda kutogusana
na udongo kitu ambacho kinaweza kusababisha tunda kuathiriwa na joto la udongo
au magonjwa kirahisi.Weka matandazo pale mche wako utakapo fikia urefu wa
sentimita 10.
Punguza urefu wa mmea
Ili kupata matunda mazuri na yenye afya ni vema kuupunguza
mmea kwa mbele ,pale unapoona mmea umefika urefu wa kutosha ili kusaidia
kutengeneza matawi ya pembeni ambayo mara nyingi ndio ubeba maua ya kike.
Kuondoa magugu
Ni muhimu sana kuondoa magugu katika shamba lako hasa wiki za
mwanzo ili kuzuia ushindani wa mahitaji
kati ya magugu na mmea ambapo hupelekea kupungua kwa mavuno na muda mwingine
magugu haya yanaweza kuwa ndio chanzo cha baadhi ya magonjwa katika mmea wako
Uchavushaji
Ili kupata kiasi kikubwa cha matunda ni
vyema kuwa na mzinga
wa nyuki karibu na shamba lako ili kusaidia uchavushaji wa maua ya
tikitimaji.Tunashauri uwe na mizinga 1-2 kwa hekari moja.Waweza pia
pands alizeti jirani na shamba lako ili kuvuta nyuki.Pia
zuia kupulizia dawa za wadudu kipindi cha maua maana unaweza wakimbiza
au kuwaua
nyuki, kumbuka maua ambayo hayakuchavushwa vizuri huzaa matunda yenye
umbo baya lisilo shabihiana na mengine.
Punguza idadi ya matunda
Kwa kawaida tikitimaji uweka zaidi ya matunda manne ,ili
kupata matunda makubwa na yenye afya ni vyema kupunguza matunda kwa kuondoa
baadhi ya matunda ambayo yanaonekana hayana afya nzuri na yaliopoteza umbo zuri
na kuhakikisha kila mche unabaki na matunda 2-3 tu.
Uvunaji
Tikitimaji uvunwa baada ya miezi miwili na nusu hadi mitatu kutoka siku ya kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.
Mangonjwa
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi
(Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na
hupendelea sana wakati wa baridi,
Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano
huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka
na madoadoa meus kwa mbali..
Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato...Metalaxyl na mancozeb ....kama
vile Ridomil gold.
2) Ubwiru juu (Powdery mildew )
Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama
yamemwagiwa unga ua majivu
Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato...Difenoconazole ..kama vile
Score.
3) Kata kiuno.(Damping off)
Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini
,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.
Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea
yako kuota.
Wadudu
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya
kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.
Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.
Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.
,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec
itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.
Mbegu bora za
tikitimaji.
Kuna mbegu chotara na opv(Sio chotara)
But mbegu bora ni chotara na baadhi ya hizo mbegu ni...
1) Arashani F1-kutoka syngenta
2) Sukari F1-Kutoka East Africa seeds.
3) Sugar king F1-kutoka africasia
4) Juliana F1-kutoka Kiboseed
5) zebra F1-Kutoka Balton.
6) Pato F1-Kutoka Agrichem
Pia zipo mbegu za Sugar king na PATO F1 250gms kwa shilingi 130,000 ambapo utapata mbegu 2,500 na matunda yake yana uzito wa kilo 3-5 na matamu sana , potable kwa kuuza na kwa kusafirisha
SOKO LA TIKITI
SOURCE: greenagricultureskills.com
Aise kwakweli nimepata elimu nzuri sana aisee
ReplyDeleteAise kwakweli nimepata elimu nzuri sana aisee
ReplyDelete