JINSI YA KUMNASA KANTANGAZE (TUTA ABSOLUTA) KABLA HAJAKULETEA HASARA SHAMBANI
MKAKATI WA KUMKABILI MDUDU “TUTA ABSOLUTA” MAARUFU KAMA KANTANGAZE
Kantangaze ni mdudu muharibifu anaependa zaidi kushambulia zao la nyanya lakini pia anaweza kushambulia viazi, hoho za njano au nyekundu, bilinganya N.k
MAISHA YA KANTANGAZE
Tuta Absoluta anakadiriwa kuwa na uwezo wa kuishi kwa siku 29 hadi 38 kutegemeana na hali ya hewa. Mdudu huyu ana uwezo wa kuzaliana kwa haraka mno. Wadudu hawa huwa hawazaliani hadi pale mazingira yanapokuwa rafiki kwa upande wao.
Jike moja la kantangaze anauwezo wa kuzalisha mayai hadi 260 kwa kipindi chote cha maisha yake.
Wadudu hawa hufanya uharibifu wakati wa usiku na kujificha kwenye majani wakati wa mchana.
NAMNA AMBAVYO ANAWEZA KUENEA
Kantangaze anaweza kuenea kwa kutumia mbegu ambazo zimeathiriwa, kutoka mmea hadi mmea, maambukizi kutokea kwenye matunda, mabaki yaliyopo shamba pia yanaweza kuathiri mazao mapya yatakayo pandwa.
UHARIBIFU NA UTAMBUZI WA UWEPO WAKE
Sehemu yoyote ya mmea katika hatua za ukuaji zinaweza kuathiriwa na mdudu huyu ingawa kantangaze hupendelea zaidi kushambulia majani na mashina ila hata matunda pia hua anashambulia
NAMNA YA KUDHIBITI
1.WEKA MTEGO UTAKAO KUWEZESHA KUTAMBUA UWEPO WAKE MAPEMA KABLA HAJALETA MADHARA
Tumia ndoo iliyo jaa maji vizuri (usijaze hadi yakamwagika) changanya maji hayo ya packt ya sabuni ya OMO, funga kamba kukatiza duara la juu la ndoo utatengeneza nusu duara mbili, chukua homone ya PHEROMONE ambayo hupatikana kwa bei ya Tsh 4000 maduka ya pembejeo za kilimo, funga homoni hiyo kati kati ya kamba kasha weka ndoo yako kati kati ya shamba
Homone hiyo hutoa harufu mithili ya jike linalotaka kupandwa hivyo kantangaze dume popote alipo shambani atajileta tu mahali mtego ulipo na utamkuta amekufa kwenye maji hayo hivyo unapaswa kuchukua hatua za haraka kuwaangamiza kabla hawajaleta madhara makubwa shambani.
Mtego huo unaweza kudumu shambani kwa muda wa siku 30 kabla ya kuwa umeisha nguvu hivyo unapaswa kurudia hatua hizo kutega upya (Angalia picha mtego huo unavyotakiwa kuwa)
2.MATUMIZI YA KEMIKALI
Matumizi makubwa ya kemikali mara kwa mara yaepukwe kwani jambo hilo hupelekea wadudu hawa kujitengenezea kinga na kuwa na uwezo wa kukabiliana na madawa hayo.
Tumia dawa itakapo bidi ila epuka kuchanganya madawa na kuyatumia kwa mara moja kwani hilo litawafanya wadudu hawa kujitengenezea kinga dhidi ya madawa.
Dawa zinazo shauriwa kutumika dhidi ya Mdudu Kantangaze
Imidacloprid
Indoxacarb
Spinosad
Deltamethrine (against adult moths)
Rynaxypyr
3.NJIA ISIYO YA KEMIKALI
Tumia mafuta ya mwarobaini (Neem Oil) ikiwa madhara ya wadudu hawa ni madogo au madhara yapo kwenye hatua za awali. Kutumia wadudu wanaokula wadudu wenzao pia inaweza ikatumika.
4.MPANGO MZURI SHAMBANI
Safisha shamba lako vizuri kabla ya kupanda ondoa masalia yote mazao shambani tumia mtego wa kantangaze mapema kabla ya kupanda ili kubaini uwepo wao mapema, fanya mzunguko wa mazao shambani, choma moto mimea yote ambayo imeonekana kuathiriwa shamabani.
KWA MAONI NYONGEZA AMA USHAURI TUNAKARIBISHA MAWAZO YA WADAU WENGINE
Source: Smart Ideas
The Golden Nugget Casino - MapyRO
ReplyDeleteThe Golden 김해 출장안마 Nugget Hotel 시흥 출장안마 and Casino is a casino in Phoenix, Arizona, 하남 출장안마 with a hotel, a casino, restaurant, live performances 동해 출장마사지 and a 경상북도 출장마사지 seasonal outdoor pool.