• UFUGAJI WA SAMAKI NA AINA ZAKE


    Aina za ufugaji
    Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake:

    1. Huria (Extensive farming)
    •    Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
    •    Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton)
    •    Hauitaji ubadilishaji wa maji
    •    Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa
     2. Kati ya huria na nusu shadidi (Modified extensive:
    •    Samaki, 4-7 kwa mita ya mraba
    •    Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika
    •    Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako
    •    Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima
    3. Nusu shadidi (Semi-intensive)
    •    Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
    •    Chakula cha asili na cha ziada
    •    Huduma ya hewa ya ziada lazima
    •    Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)
    4. Shadidi (Intensive)
    •    Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
    •    100% chakula cha kutengenezwa
    •    Maji ni kuingia na kutoka
    •    Hewa ya ziada masaa yote
    •    Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine
    Miundombinu ya ufugaji
    Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo
    Bwawa
    •    Kina 0.8-1.5m
    •    Ukubwa 100 mita za mraba- 1ha
    Matanki
    •    Umbo-mstatili au mviringo nk
    •    Kina 1-1.5m
    •    Kipenyo kwa lile la mduara 3-10m
    •    Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
    Materials: Plastic, cement, chuma nk
    NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)

    Vizimba (Fish cages)
    •    Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium.
    Eneo linalofaa kwa ufugaji
    Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:
    1.    Udongo: Mfinyanzi husaidia kupunguza gharama za ujenzi wa bwawa na maji kwakuwa linaweza kutuamisha maji na kuruhusu maji yasipotee. Likiwa la kichanga bwawa ni lazima lijengewe au kuwekwa nylon sheet ili kuzuia upotevu wa maji. Unaweza ukahamisha udongo wa mfinyanzi kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kuzuia upotevu wa maji (muone mtaalamu kwa ushauri zaidi juu ya mbinu ya kuhamisha udongo).
    2.    Chanzo cha maji ya uhakikaEneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.
    3.    Miundombinu ya barabara: Inasaidia kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na samaki wakati wa kuvuna.
    4.    Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako. Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
    5.    Eneo lenye mwinuko wa wastani husaidia katika ujenzi wa bwawa.
    6.    Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
    7.    Ulinzi ni muhimu
    Angalizo: Aina ya eneo lako ndilo linaweza kukufanya uchague muundombinu gani wa kufugia utumie

    Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa
    Maji baridi
    Sato/Perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout
    maeneo ya baridi kama vile
    •    Iringa
    •    Kilimanjaro
    •    Arusha
    •    Mbeya
    Maji bahari
    Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu

    Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika
    Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika vituo vya kuzalishia vifaranga.

    Sato na Kambale. Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.
    Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex).
    •    Kingolwira - Morogoro
    •    Luhira - Songea
    •    Mbegani - Bagamoyo .
    Vituo binafsi kama vile Faith aquaculture-Kibamba (DSM) (utapata monosex sato), Peramiho Songea (mixed sex). Monosex huuzwa Tsh. 200 kwa kifaranga, na mixed ni100 kwa kifaranga.

    Trout
    Mayai huagizwa toka Marekani, Israel
    Kambamiti wa baharini Alphakrust “Mafia.

    Chakula cha samaki
    Chakula cha asili
    Hurutubishwa kwa mbolea ya wanyama kama vile kuku, ngombe, mbuzi nk. Kwa kiwango cha 1000kg/ha. Mbolea ya kuku ni kali hivyo unaweza punguza ikawa 250-500kg/ha.

    Chakula cha kutengeneza
    Samaki huitaji protein ili akuwe na kila samaki ana mahitaji yake hivyo ni species specific. Formula zipo kwa wale wanaotaka kutengeneza. Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza. Ingredients zake ni kama vile dagaa, pumba, soya, unga wa ngano, unga wa muhongo nk.

    Uvunaji
    Kwa kawaida ni miezi 4-6 amabapo unapata 250-400g kulingana na ulishaji wako. Kwa prawns ni miezi 3-6 wanafikia 30-50g ambayo ni ukubwa wa soko.


    Tathmini ya uchumi
    Perege/Sato Mfano:
    Ukubwa wa bwawa ni 20m by 30m= 600 mita za mraba
    Idadi ya samaki (7 kwa mita ya mraba) kwa monosex tu= 600 x 7=4200 fish
    Uzito hadi kuvuna (4-6months)- 250g= 4200 x 250g= 1050kg (Nimesha convert gram to kg) Bei kwa kilo ni 6000-8000 kulingana na mahali= 6milion-8milion.

    Gharama unazoweza kutumia
    Ujenzi wa bwawa
    Kuchimba kwa vibarua ni 500,000-600,000
    Kuchimba kwa machine ni 1,000,000-1,500,000 kulinganana mahali ulipo

    Kama udongo ni kichanga itabidi ujengee (kujengea ni gharama na inaweza ikafika3.5-4m kwa gharama zote kuanzia kuchimba hadi kujengea).

    Chakula cha kutengeneza tani 1 inaweza kugharimu laki 7-9. Hapa ili uweze kuzalisha tani 1 ya samaki aina ya perege utahitaji tani 1-1.5 ya chakula.
    Gharama ya vibarua 150,000-250,000 kwa mwezi.
    Utakuwa na gharama ya chokaa kwa ajili ya kuua vidudu (100,000-200,000), mbolea kuzalisha chakula cha asili (gharama ni 50,000).

    1 comment: