BATA BUKINI: UFUGAJI WENYE TIJA
KUTAGA
Bata Bukini huanza kutaga baada ya miezi saba na hutaga
mara tatu kwa mwaka. Isipokuwa, utagaji wa bata bukini weupe na wa
rangi hutofautiana katika idadi ya mayai
Bata Bukini weupe hutaga mayai sita tu lakini wale wa mchanganyiko wa rangi hutaga mayai kumi na mbili (mara mbili ya weupe)
KUATAMIA
Jinsi ilivyotofauti katika idadi ya utagaji wa mayai
hivyo ndivyo uwezo wa kuatamia pia ulivyo. Bata Bukini weupe huatamia
mayai 6 na wale wa rangi huatamia mayai 12
Ndege hawa huatamia kwa
siku 29, huangua vifaranga kwa siku 3 na mara nyingi hutotoa mayai yote,
si rahisi mayai kubaki bila kutotolewa au kuharibika.
NAMNA YA KUTUNZA VIFARANGA
Mara tu vifaranga wanapoanguliwa, wachukue na kuwatenga na mama yao
kisha waweke katika banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea
taa ya umeme kama una uwezo ili kuwatengenezea joto.
Pia, waweza kuzungushia banda lao kitu kizito kama blanketi ili kuwakinga na baridi au upepo.
BANDA
Bata Bukini wanahitaji nafasi ya kutosha hivyo andaa banda kulingana na wingi wa bata unaotarajia kufuga.
Hakikisha banda limesakafiwa au banda la udongo lisilotuamisha maji au
unaweza kuweka mbao au mabanzi kisha unaweka maranda ili kuwakinga na
baridi.
MAJI
Ni lazima bata wapatiwe maji ya kunywa kila siku
na hakikisha banda halikosi maji wakati wote. Safisha chombo cha maji
na kubadilisha maji kila siku.
Ndege hawa wanahitaji maji ya
kunywa ya kutosha kama ilivyo kwa kuku. Hakikisha maji yako kwenye
chombo ambacho hayatamwagika , kwani kumwagika kunaweza kusababisha
kuibuka kwa magonjwa. Bata Bukini hawapendi uchafu. Hivyo maji yawe mahali ambapo hayatachafuka.
SOURCE: FREBU Poultry Farm
Mnapatikana wap ili kupata mbegu ya bata bukini
ReplyDelete