• UFUGAJI WA BATA BUKINI WENYE TIJA: SEHEMU YA KWANZA

    BATA BUKINI
    UFUGAJI WENYE TIJA
    Tofauti na ndege wengine au bata wengine wa kawaida, mfugaji wa bata bukini anaweza kupata kipato kikubwa kwa haraka na kwa gharama ndogo.
    Bata Bukini ni ndege ambao asili yao ni India na Japan. Hii ni jamii ya ndege wafugwao lakini tofauti kubwa ya bata wa kawaida wao wana asili ya usafi, hivyo hawapendi uchafu na kamwe hawali mizoga.
    Kuna aina mbili ya bata bukini ambao ni weupe na wenye mchanganyiko wa rangi. Hali kadhalika hutofautiana katika utagaji wa mayai.


    CHAKULA
    Ndege hawa wanakula chakula kama wanacholishwa kuku, wanapendelea kula majani jamii ya mikunde kwa 50% na hawahitaji chakula kingi. Vifaranga ni lazima wapatiwe lishe kamili hasa protini kwa wingi ili waweze kujenga mwili, kukua vizuri na kuwa na afya nzuri.
    Kwa maana hiyo, vifaranga wanahitajika kupata walau 20% ya protini kwa wiki mbili za awali na baada ya hapo waweza kupunguza hadi 15% kulingana na kukua kwao hadi wanapokuwa wanaelekea kukomaa.
    Kama ambavyo mfugaji anaweza kutengeneza chakula kwa ajili ya mifugo wengine, pia anaweza kutengeneza cha bata bukini kama ifuatavyo:
    Mahitaji
    🐥 Mahindi kilo 10 ( hakikisha hayana dawa)
    🐥 Chokaa kilo 5 (ya kulishia mifugo)
    🐥 Dagaa kilo 10 (wanaotumika kulishia kuku)
    🐥 Mashudu kilo 20
    Utengenezaji na Uhifadhi
    Baada ya kupima vyakula hivi kwa usahihi chukua pipa, changanya vizuri kisha walishe bata kulingana na wingi wao na uhakikishe wanapata chakula cha kutosha. Vipimo hivi hutegemea wingi wa bata unaowafuga lakini hakikisha uwiano huo unazingatiwa. Baada ya kutengeneza chakula unaweza kuhifadhi katika mifuko na kuweka katika eneo lisilokuwa na unyevu.





    SOURCE: FREBU Poultry Farm

    No comments:

    Post a Comment