MAGONJWA
Ni mara chache sana bata bukini kushambuliwa na magonjwa kama watawekwa katika hali ya usafi. Magonjwa yanayoweza kuwasumbua ni mafua na wakati mwingine kuharisha
TIBA ZA ASILI
Unaweza kutibu bata bukini kwa njia za asili. Tumia mwarobaini, vitunguu (maji na saumu).

Maandalizi
Chukua kiasi kidogo cha mwarobaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji ya mwarobaini, kisha changanya na maji uliyo andaa kuwanywesha vifaranga.

Dawa hii hutumika kukinga na kutibu bata bukini wanaoharisha.
Maandalizi
Unachukua kitunguu saumu au maji na kuondoa maganda ya nje kisha safisha na kukata vipande vidogovidogo na kuwawekea kama chakula.Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapopona.

SOURCE: FREBU Poultry Farm
No comments:
Post a Comment