WADUDU WAHARIBIFU.
1. Minyoo (Root-knot nematodes):
Huenezwa na minyoo jamii ya Meloidogyene incognita, M. javanica, M.arenaria na M.halpa.
KINGA.
Tumia mzunguko wa mazao yanayostahimili minyoo. Hasara hufikia 15%-40%
ya mavuno. Hasara huweza fikia 90% ya mavuno endapo minyoo itashambulia
kwa wingi. Kwa hali kama hii itakubidi kuhama eneo.
2. Utitiri wa mhogo.(Cassava green mites).
Wadudu hawa pia huitwa Mononychellus tanajoa. Hasara itokanayo na wadudu hawa hufikia 20% - 80% ya mavuno ya mwaka. Kinga...
1. Tumia mbinu za kibaiologia kwa kuwahusisha wadudu kama Typhlodrimalus aripo ambao huwatafuna.
2.. Panda mbegu ya pingili kutoka katika mimea isiyoshambuliwa..
3. Badilisha mazao katika shamba.
VIDUN'GATA (Cassava Mealybug);
Mdudu huyu hujulikana kitaalamu kama Phenacoccus manihot. Mdudu huyu
ameenea Tanzania nzima na huleta hasara ya wastani wa 75% kwenye zao
hili. Mdudu huyu hudumaza utokaji wa ncha ya mmea na kuufanya ufe.
Vidung'ata hutafunwa na wadudu kama vile Hyperapsis notata na Diomus sp.
Vidung'ata huzuiliwa vile vile kwa kutumia manyigu aina ya Apoanagynus
lopezi, wanaozalishwa kwenye maabara (mfano.. Taasisi ya Utafiti wa
Sukari - Tumbi Kibaha) nk..
MAGONJWA.
Mhogo hapa Tamzania hushambuliwa na magonjwa makuu manne;
1. Batobato -afrikan cassava mosaic,
2. Cassava brown streak.
3. Cassava bacterial blight.
4. Kuoza ardhini.
KINGA
1. Panda pingili safi zisizokuwa na ugonjwa.
2. Panda mbegu kinzani yaani zinazovumilia magonjwa na eneo husika mfano .. kibaha, kigoma nyekundu, mulundi nk..
3. vuna mapema haswa kwa aina kama kiroba-Rufiji na Mtwara.
4. Katika vituo vya utafiti ugonjwa huweza kuzuiliwa kwa kuwa
kuzichovya pingili ndani ya madawa kama vile Rogor 40% ECna Dithane
M-22.
KUVUNA/KUHIFADHI.
Mhogo kwa kawaida huvunwa ukiwa na
umri wa miezi 6 -10- hadi 24 kutegemeana na mbegu na hali ya ardhi.
Uvunaji wa majani kama mboga Huweza kuanza siku 50 hadi 70 tangu
kupandwa.
Mhogo waweza kuifadhiwa kwa kusitisha kuivuna shambani.. kuisindika au kwa kuichimbia chini ya ardhi.
Inashauriwa mihogo itengenezwe mara tu baada ya kuvunwa..
Hapa Tanzania hekta moja ya mhogo huweza kuzalisha kati ya tani 4 - 10 za mhogo.
Karibuni ndani ya FREBU
Tupambane na changamoto ya ajira, tuhakikishe kuwa tunaimarisha uchumi wetu na kutengeneza ajira nyingi ndani ya jamii yetu
SOURCE: FREBU Poultry Farm
No comments:
Post a Comment