• KILIMO BORA CHA MIHOGO KWA AJILI YA BIASHARA: SEHEMU YA KWANZA

    KILIMO CHA MHOGO (Cassava - manihot exculenta).
    Mhogo umefahamika na kutumika huko Amerika ya Kusini zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Iliketwa Afrika na Wareno kupitia Congo mwaka 1588. Mhogo umeanza kutumika katika Afrika Mashariki kuanzia karne ya 18.


    Kuna aina kuu mbili za mhogo.
    1.Mhogo mtamu na
    2. Mhogo mchungu.
    Mhogo mtamu unaweza kuliwa mbichi, kuchemshwa, kuchomwa, kuokwa mikate na keki na kukaangwa (chips dume) nk.
    Aidha mhogo mchungu lazima usindikwe ili kupunguza sumu iliyopo na kisha kukaushwa kuwa makopa na kutumika kwa ugali..uji..au viwandani.
    Majani ya mhogo ni mboga nzuri (kisamvu) na miti yake huweza kutumika kwa kuni. Mhogo uliokaushwa hutumika vilevile kwa malisho ya mifugo haswa nguruwe.

    AINA YA MIHOGO.
    Kuna zaidi ya aina 200 za jamii ya mihogo, lakini Manihot esculenta (Cranz) ndio inayotumika kwa chakula na kwenye viwanda.
    Wakulima wengi hutumia mbegu za kienyeji. Kati ya hizo mbegu zinazopendekezwa ni pamoja na liongo kwimba, aipin valenca, msitu zanzibar, kigoma, mapambano, kigoma nyekundu, kibandameno, nk.

    UZALISHAJI.
    Mihogo hulimwa kwa wingi katika mikoa yote ya ukanda wa Pwani na Zanzibar na kwenye ukanda wa maziwa ya nyanda za Tanganyika na Nyasa.
    Takwimu za Shirika la Kilimo miaka ya nyuma zilikuwa zikikuwa zikionyesha kuwa nchi za Nigeria, Kongo/Zaire, Mozambiki, ndizo zinazolima mihogo kwa wingi barani Afrika. Wakati Naigeria huvuna tani milioni 31.5, Congo tani milioni 18, Mozambiki Tani milioni 4.7 Cameroon huvuna tani milioni1.3, Tanzania huvuna tani 591,200 tu kwa msimu.

    MAZINGIRA RAFIKI YA MHOGO.
    Katika tropiki (latitudo 30°N na 30°S)

    JOTO.
    Joto lisipungue nyuzi joto 20 °s . Kwa kawaida mihogo haistahimili baridi wala ukungu.

    MVUA.
    Kati ya mililita 500 - 2500 kwa mwaka.

    UDONGO.
    Mihogo hustawi kwenye ardhi isiyokuwa na rutuba nyingi. Udongo usiotuamisha maji na uwe wenye kupitisha hewa kwa urahisi na usiwe na chumvi nyingi.
    Lima shamba kwa kina cha jembe, safisha vichaka na panda. Utifuaji mzuri husaidia kupata mizizi mingi na mikubwa.

    KUPANDA.MBEGU.
    Mihogo hupandwa kwa kutumia pingili za urefu wa sm 15 hadi sm 30. Pingili hizi ziwe na takribani macho matano na zikatwe kutoka katikati ya shina badala ya sehemu ya juu
    Pingili zichomekwe ardhini nusu ya urefu wake.

    NAFASI.
    Nafasi ya kupanda iwe sm 90 kwa 150 au sm 75 kwa 150 kwenye tuta. Aidha kwa kuzingatia upana wa kivuli kulingana na aina ya mhogo unaokusudiwa kupandwa, wakulima wengi hutumia nafasi ya sm 100 kwa 100.
    Kwa mpando wa sm 90 wa sm 90/150 unajitaji pingili 9260 kwa hekta moja , na pingili 8880 kwa mpando wa 75/150 sm kwa hekta 1.

    MSIMU WA KUPANDA.
    Mhogo unaweza kupandwa wakati wowote kukiwa na unyevu nyevu ardhini.

    UTUNZAJI.
    Mhogo huhitaji palizi, mara 2-3 katika kipindi cha miezi 3-6 tangu kupandwa kwake. Changanya zao la mananasi na kunde ili kupunguza gharama za palizi.
    Kwa matumizi ya majani kisamvu inashauriwa kuimwagilia maji mihogo yako wakati wa kiangazi. Samadi au mboji huwekwa shambani haswa pale mkulima anapokuwa na nia ya kuvuna majami kwa ajili ya mboga ya kisamvu.




    SOURCE: FREBU Poultry Farm 

    No comments:

    Post a Comment