• JE UNAFAHAMU MAGONJWA MBALIMBALI YA MBWA NA JINSI YA KUYADHIBITI: SEHEMU YA KWANZA

    MAGONJWA YA MBWA
    Mbwa ni mnyama muhimu sana katika maisha ya binadamu kwani mnyama huyu husaidia katika ulinzi na mapambo katika nyumba, hivyo basi kumtunza mbwa ni jambo la msingi sana ikiwemo udhibiti wa magonjwa na wadudu wasumbufu pamoja na maradhi (nyumba/banda), hivyo basi yafahamu magonjwa na wadudu wasumbufu wanaosumbua mbwa zaidi.



    1. KICHAA CHA MBWA (RABIES)
    Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoambukizwa kutoka kwa wanyama hadi binadamu kupitia mate, kwa kung`atwa na mbwa mwenye maambukizi ya virusi vya kichaa.
    Ambapo mbwa au mnyama aliye patwa na virusi hivi akimng`ata mtu au mnyama mwingine asiye kuwa na kichaa humuambukiza.
    Kichaa hupatwa kwa wanyama walio kundi la mamalia, kwa paka wao wanaukinzani kidogo na ugonjwa huu kulinganisha na mbwa.
    Mara baada ya kuumwa waweza usione dalili za ugonjwa huu, kwani huchukua muda, kulingana na sehemu uliyo umwa hadi kufikia katika ubongo.

    Dalili za awali za kichaa cha mbwa.
    (a) Mbwa kujikuna mara kwa mara.
    (b) Mbwa kutokwa na mate mengi mdomoni.
    (c) Mnyama kupoteza hofu ya kitu chochote.
    (d) Mnyama kung`ata vitu ovyo ovyo.
    (e) Mnyama kuzunguka ovyo
    (f) Mbwa kutopenda mwanga na kukaa gizani.
    (g) Mbwa kuogopa maji.
    (h) Mbwa kubadili tabia, mbwa mkali kuwa mpole na mpole kuwa mkali ( mbwa huwa na tabia zisizo za kawaida.)
    (I) Mbwa kukojoa mara kwa mara.
    (j) Mbwa kutopenda vitu alivyovizoea.
    Dalili za baadae za kichaa cha mbwa.
    (a) Mnyama kupoteza fahamu.
    (b) Mnyama kupooza baadhi ya viungo.

    KUDHIBITI
    (a) Mpe mbwa wako chanjo kila baada ya muda wa mwaka mmoja.
    (b) Kwa mbwa waliokwisha pata kichaa cha mbwa hakikisha wanadhibitiwa vya kutosha, kwani mbwa waliopata kichaa huchukua siku tatu hadi kufa.
    (c) Dhibiti mbwa wanaozurula mtaani (zuia mbwa wa mtaani.)
    (d) Jina la chanjo ni RABIES .

    2. UGONJWA WA MFUMO WA HEWA.
    Huu ni ugonjwa unao athiri mfumo wa hewa ikiwemo TB, Phnemonia, ni magonjwa yanayo sambaa kutoka mnyama mmoja kwenda mnyama mwingine kwa njia ya hewa.

    Dalili zake,
    a) Upumuaji wa shida.
    b) Mbwa kushindwa kupumua.
    c) Kupumua kwake kunatoa sauti nzito, ile ya kukoroma.
    d) Mbwa kukohoa.
    e) Mbwa hupumzika mara kwa mara.
    f) Mbwa kutoweza kubweka.
    g) Kutoka mapovu puani au ute.

    Tiba.
    h) Mpe mbwa wako dawa yeyote ya Atibiotic kama, OTC, penstrep, Tirosin.
    i) Pamoja na dawa ya vitamini ambayo itamsaidia kurudisha hamu ya kula.

    3. MINYOO (WORMS)
    Minyoo ni wadudu wanaosumbua kwa kiasi kikubwa sana katika mbwa hata kwa wanyama wengine wengi wafugwao kama mbuzi, ng`ombe na kondoo, ambapo huweza sababisha madhara makubwa katika mbwa na kupelekea mbwa kudumaa na hadi kufa.

    Dalili za Minyoo katika mbwa ni,
    a) Kuharisha.
    b) Mbwa kupoteza hamu ya kula.
    c) Manyonya kusambaratika.
    d) Uzito kushuka.
    e) Mbwa kuwa dhaifu.
    f) Mbwa kukohoa
    Wafuatao ni aina ya minyoo wanao sumbua sana katika mbwa.
    1. Minyoo wa mviringo.
    2. Minyoo wa kwenye moyo.
    3. Minyoo wa kwenye mapafu.

    Tiba
    Fanya chanjo za minyoo kwa kila baada ya muda wa miezi mitatu, na kwa wale ambapo tayari wamepata ugonjwa wa minyoo wapatiwe dawa ya minyoo ambayo ni IVERMECTIN.

    4. UKURUTU (MANGE)
    Ugonjwa wa ngozi, na ugonjwa huu uweza kutoka kwa mnyama mmoja kwenda mnyama mwingine, pia hata kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

    Dalili.
    a) Mbwa kujikuna kupita kiasi.
    b) Manyoya kunyonyoka.
    c) Gamba gumu hujitengeneza juu ya ngozi.
    d) Eneo lililoathirika huwa na gamba gumu.
    e) Mnyama anakuwa anajikuna mara kwa mara.

    Udhibiti.
    a) Ogesha mbwa wako mara kwa mara angalau mara tatu kwa kila mwezi, hii itasaidia mbwa kutopata ugonjwa wa ukurutu.
    b) Tenga mbwa waliopatwa na ukurutu.
    c) Kwa mbwa waliopata tayari ukurutu wapatie dawa ya IVOMECTIN dawa hii imeonesha mafanikio makubwa katika kutibu ukurutu na dawa hii huchomwa katikati ya ngozi na nyama.




    SOURCE: FREBU Poultry Farm

    No comments:

    Post a Comment