• JE UNAFAHAMU MAGONJWA MBALIMBALI YA MBWA NA JINSI YA KUYADHIBITI: SEHEMU YA PILI





    5. UGONJWA WA KUTETEMEKA (CANINE DISTEMPER).
    Huu ni ugonjwa unaosambaa kutoka mnyama mmoja kwenda mwingine, na ni ugonjwa unapelekea vifo vya mbwa wengi. Ni ugonjwa wenye chanjo zake.
    Ugonjwa huu husababishwa na virusi wanaoitwa Canine Distemper Virus(CDV)

    Dalili za Ugonjwa.
    a) Mgonjwa kutetemeka
    b) Mbwa kupooza miguu ya nyuma.
    c) Anapunguza kula.
    d) Macho yanavimba hadi upofu.
    e) Ute ute mwingi kutoka kwenye pua.
    f) Kuharisha
    g) Dalili ya mwisho mbwa kupooza mwili

    Udhibiti.
    a) Ugonjwa huu hauna tiba bali ni chanjo inayoitwa DHLP.
    b) Chanjo hii apewe mbwa akiwa na umri wa wiki 8 hadi wiki 12.

    6. WADUDU WASUMBUFU.
    Mbwa akiwa na wadudu hawa hujikuna sana na hujikuna mara kwa mara hasa hasa sehemu za mkia, pia mbwa hukosa raha na muda mwingi hupoteza hadi hamu ya kula kwa usumbufu huu wa wadudu, wadudu hawa sumbufu ni kama viroboto, kupe, chawa na papasi.

    Udhibiti.
    - Jinsi ya kudhibiti wadudu hawa ni kuogesha kwa kutumia dawa maalumu Dog shampoo, tik tik na paranex. Kwa dog shampoo imeonyesha kufanya vyema sana kwa kudhibiti na kuua kabisa.
    - Usafi wa nyumba wanazo ishi mbwa ni muhimu sana kwa kuwa huku ndiko usafi usipo zingatiwa wadudu hawa huzaliana kwa wingi sana, safisha kwa maji safi pamoja na kutumia dawa maalumu ili kudhibiti wadudu hawa, hakikisha dawa unachanganya kwa usahihi bila kuzidisha kwani uweza pelekea mbwa kudhurika.

    7. VIRUSI VYA PARVO.
    Ugonjwa huu (virusi vya parvo) huwakumba sana watoto wa mbwa wenye umri wa kuanzia wiki 2 hadi wiki 4. Husababishwa na virusi aina ya Canane parvo virus

    Dalili,
    a) Kuharisha.
    b) Kutapika.
    c) Wanakosa hamu ya kula.

    Tiba
    a) DHLP ni chanjo inayotumika kudhibiti ugonjwa huu.
    b) Antibiotic kama OTC hutumika kwa kutuliza tu na sio kutibu magonjwa.







    SOURCE: FREBU Poultry Farm

    No comments:

    Post a Comment