• KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI

    KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
     


    UTANGULIZI
    Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua (ingalau kiasi cha masaa 6 kwa siku)
    Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
    Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.

    KUANDAA MICHE
    Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi 10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishi shambani.

    KUHAMISHA MICHE SHAMBANI
    Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaid haitapelekea shida yoyote.

    MUHIMU...Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia mambo yafuatayo.
    Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.
    Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche kisha changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri wa kuhamisha miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho jua limefifia kuepuka miche kukauka.
    Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata virutubisho.
    Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.

    MAHITAJI YA MMEA
    Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji yasiwe yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka. Epuka umwagiliaji ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Mau ya mmea hua na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza kujichavusha yenyewe. Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza uchavushaji.

    KUPALILIA
    Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia kuepuka kukata mizizi.

    MAGONJWA
    Pilipili inaweza kushambuliwa na magonjwa yafuatayo, blossom end rot, anthracnose, tobacco mosaic virus, bacterial spot, and mildew. Namna ya kulinda mimea yako dhidi ya magonjwa hayo weka shamba lako katika hali ya usafi na ondoa magugu shambani kuondoa sehemu za mazalia ya wadudu. Ondoa mimea iliyo athiriwa kabla ugonjwa haujasambaa shambani.

    MAVUNO
    Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi 1 hadi 3.


    USALAMA WAKATI WA UVUNAJI
    Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
    kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye macho.

    SOKO
    Fursa

    Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute) hivyo kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.
    Changamoto
    Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi huathiri sana soko la pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana haiwezi kushawishi watumiaji kutumia pilipili nyingi zaidi.
    Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza huduma shambani hadi pale soko litakapo tengemaa vizuri.
    MBINU ZA MAFANIKIO KWENYE KILIMO

    1. ZALISHA KWA WINGI
    Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.

    2. TAFUTA MASOKO YA BIDHAA KABLA YA KUANZA UZALISHAJI
    Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako. Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza wateja na wateja watakutengenezea biashara.
    Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.
    -Unafuu wa bei
    -Ubora wa zao
    -Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
    Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa umejihakikishia soko la uhakika

    3. USILIME KWA KUFUATA MSIMU
    Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara muda mwingine.
    Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.
    (FANYA KILIMO CHA UMWAGILIAJI)

    4. USIFANYE KILIMO KWA MAZOEA
    -Tumia wataalamu wa kilimo
    -Tumia njia za kisasa za kilimo
    -Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia wataalamu)
    -Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri zaid

    FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI
    1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu
    2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.
    3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.
    4. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili
    5. Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!
    6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)
    7. Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.
    8. Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu

    NOTE; Kula kupita kiasi ni hatari pia kwa afya yako

    KWA MAONI NYONGEZA AU USHAURI TUNAKARIBISHA MAWAZO YA WADAU WENGINE: VILE VILE USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK
    =====>Mabusi H.M Agricultural Projects






    Source: Smart Ideas

    No comments:

    Post a Comment