• KILIMO BORA CHA PILIPILI KICHAA (AFRICAN BIRDS-EYE CHILI)

    KILIMO BORA CHA PILIPILI KICHAA (AFRICAN BIRDS-EYE CHILI)
     


    UTANGULIZI
    Pilipili ni aina ya pilipili kali. Hustahimili hali ngumu ya
    kimazingira na hazina magonjwa na wadudu wengi. Hali hii hufanya gharama ya ukuzaji
    kuwa chini zaidi kushinda mimea mingine. Pilipili kichaa ina wingi wa vitamin A na C na
    hutumika kama kiungo kwa chakula. Pia inaweza kukaushwa.

    HALI YA HEWA

    Huvumilia hali nyingi ikiwemo; joto na ukame ukizingatia
    unyunyizaji maji. Hata hivyo hali nzuri kwa mmea huu ni uvuguvugu na joto.
    Pia inahitaji mvua ya kadri kati ya 600mm – 1200mm kwa mwaka.
    Hali ya maji mengi mchangani hata kwa mda mchache husababisha kuanguka kwa majani.
    Pia upande mwingine ukame husababisha kuanguka kwa maua kwa hivyo nyunyiza maji.
     
    AINA YA UDONGO
    Hufanya vizuri katika aina tofauti za udongo, lakini zingatia usiwe udongo wa kutuamisha maji.
    Mmea huu hufanya vizuri unapotumia samadi.
     
    MBEGU
    Tumia mbegu iliyothibitishwa na kampuni ya MACE FOODS LTD. Nao kampuni hii
    hununua hili zao.
     
    KUTAYARISHA KITALU
    Weka kitalu mita moja upana kwa urefu upendao kulingana na mbegu yako.
    Elekeza kitalu chako upande ambao jua lisiunguze miche.
    Piga mistari ya 10 cm na weka mbegu, funika udongo kidogo. Weka manyasi makavu na nyunyizia maji asubuhi na
    jioni.
    Zinapoanza kuota, ondoa nyasi na weka kivuli mita moja juu na endelea kunyunyizia maji.

    KUPANDA
    Panda kachachawa miche ikiwa na majani halisi manne. Itakuwa imefika wiki sita.
     
    PALIZI
    Palilia mara mbili kwa msimu kuapata mavuno mengi zaidi
    Kwa mazao bora panda mmea huu pekee yake 1 meter x 1 meter. Lakini ukitaka unaweza kuchanganya na mmea mingine.
    Weka samadi na baada ya wiki moja weka DAP kuongeza rutuba ya udongo. Pia weka CAN baada ya wiki tatu zaidi.

    KUHIFADHI UNYEVU
    Tandika manyasi makavu ili kuhifadhi unyevu na kuthibiti hali ya joto la udongo.
    Tunashauri kuonana na wataalamu wa kilimo kwa ushauri zaid ili kilimo chako kiwe chenye tija zaidi.

    KWA MAONI USHURI AU NYONGEZA TUNAKARIBISHA MAONI YA WADAU WENGINE :        VILE VILE USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK
    =====.> Mabusi H.M Agricultural Projects









    Source: Smart Ideas

    No comments:

    Post a Comment