UFUGAJI NI SULUHISHO KWA TATIZO LA AJIRA
Kwa miaka mingi nchini Tanzania, na katika baadhi ya nchi nyingine za
mashariki mwa Afrika, shughuli za kilimo na ufugaji zimekuwa zikichuku-
liwa kuwa ni shughuli za wazee na watu wasio kuwa na uwezo hasa waishio
viji- jini, huku vijana wakikimbilia kazi za kuajiriwa maofisini na
kwenye biashara mijini. Kutokana na hali hii uzalishaji wa chakula na
mazao ya biashara ulishuka kwa kiasi kikubwa sana, na kusababisha bei ya
vyakula na mazao ya mifugo kuwa ya bei kubwa kutokana na uhaba. Hali
hii pia ilisababisha kuyumba kwa uchumi katika maeneo husika. Watu wenye
kipato pia wakitumia fedha nyingi kununulia chakula na mazao ya mifugo
na maskini wakiendelea kuwa na maisha duni, na afya hafifu kwa kutoweza
kumudu kupata lishe kamili kama inavyotakiwa. Kwa kuwa sekta hii ni
muhimu na inategemewa na kila mtu ingawa haiku- pewa kipaumbele, hali ya
uchumi mijini pia ilibadilika na kusababisha vijana walio wengi ambao
walikuwa waki- kimbilia humo kujipatia ajira kukosa fursa hiyo. Na hapa
ndipo ule usemi usemao shida ni mwalimu mzuri ulipo- chukua nafasi
yake. Hivi sasa, wimbi la vijana wanaofanya shughuli za kilimo na
ufugaji, limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Hii inatokana na ukweli
kwamba kilimo na ufugaji ndiyo sekta pekee ambayo ina ajira ya uhakika,
na uweze- kano wa kujipatia fedha kwa mwaka mzima ni mkubwa mno.
Tumeshuhudia na kusikia kwa siku za karibuni, vijana wanavyohangaika
kupata fursa za kujipenyeza kwenye kilimo, na kuweza kufanya shughuli
hii kibiashara. Tunawapongeza wale wote ambao wameweza kugundua kuwa
kilimo na ufugaji ni kazi ya heshima na yenye tija kubwa kwa maisha yao.
Pia tunawatia shime wale wote ambao bado hawa- jaanza wafanye hivyo,
kumbuka, jembe halimtupi mkulima.
SOURCE: Kuku project
No comments:
Post a Comment