• SUPERLISHE MCHICHA

     SUPERLISHE MCHICHA


    Swala la ukosefu wa ajiri ni moja ya changamoto zinazozikabili dunia kwa muda mrefu sasa.Kutokana na changamoto hii watu wengi wamejaribu kujiajiri wenyewe ili kujipatia ajira zao pia kuwa vyanzo vya ajira kwa jamii inayoizunguka.
    Kama alivyo sema Sir Richard Branson kwamba fursa za biashara ni kama mabasi mda wowote kuna ambayo inakuja basi leo tunakuletea fursa hii ya mchicha super lishe kibiashara ambayo kwa wale ambao hawana biashara wanaweza iangalia kwa mapana nakuona jinsi gani waweza kuifanya kama ikitokea ikawa ni moja ya fursa uliyoipenda.
    Pia kwa wale wenye biashara au ajira za muda mrefu au ajira fupi nitaungana na msemo mmoja aliowahi sema nguli wa uwekezaji duniani Mzee Warren Buffet kwamba suitegemee njia moja ya kukupatia kipato bali tengeneza au buni njia nyingine za kukuongezea kipato chako.

    SUPER LISHE
    Mboga hii ya majani imekuwa ni mboga inayolimwa sehemu nyingi duniani.Nazaidi yayote imekuwa ikitumiwa na watu wengi duniani.Zipo faida nyingi sana kitabibu ambazo zimezidi kuongezea umaarufu na kufanywa mboga hii kutumiwa kwa wingi duniani.

    SUPER LISHE KIBIASHARA
    Utafiti uliofanyika unaonesha kwamba kilimo hichi kwa hapa Tanzania zimekuwa zikilimwa katika kiwango kidogo na madhumuni yake yakiwa kutengeneza faida ndogo.Ni wachche walioweza fahamu kuwa Superlishe inaweza kuwa ni moja ya ajira yako njema.
    Utafiti tulioufanya tumegundua kuwa kilimo hichi cha mchicha Super lishe kikifanyika kibiashara kwa kuanza na hekari moja unaweza kutengeneza kipato kikubwa sana.
    Mahesabu yetu yalianza kwa kuzingatia vigezo vifutavyo:

    •    ENEO
    Hapa tulifanya utafiti wa eneo moja ambalo la kuweza anza fanya biashara hii ni ukubwa wa hekari moja ambao unaeneo za mraba 4046.86.

    •    MATUTA
    Katika ukubwa huu wa hekari moja kwa ukubwa watuta zenye urefu wa mita 30 kwa upana wa mita 3 itakuwa na eneo la mraba 90.Sasa katika hesabu za kawaida ni kwamba katika eneo la mraba 4046.86 tukiligawa katika eneo la mraba 90 tutapata matuta 44.Lakini tukitoa matuta 4 kwa mlinganisho wa ile mistari inayotenganisha tuta na tuta basi tutabakiwa na matuta 40.

    •    MBEGU
    Mbegu za mchicha kwa kilo za super lishe bei ya rejareja ni shilingi 5000 za kitanzania.Mbegu 1kg kwa makadirio ya tuta mbili.Ambayo kwa uhalisia ni kadirio la juu la mbegu ili kupunguza usumbufu.Katika matuta 40 inamaana zitahitajika mbegu kilo 20 za mbegu ambayo ukizidisha na bei ya manunuzi ya 1kg utapata shilingi 100000(laki moja) za kitanzania.

    •    MAJI
    Swala la maji ni muhimu sana.Sababu kilimo hichi kitakuwa ni cha muda mrefu yaani ni shughuli unayoweza ifanya mwaka mzima basi ni vyema ukazingatia upatikanaji wa maji.Maji yanaweza patikana kama uko karibu na vyanzo vya maji au kwa kuchimba visima.
    Changamoto inayowakabili wengi kwa sasa ni kwamba walimaji wengi wadogo wadogo hasa kwa mikoa ya dare s salaam wanalima mabondeni sehemu ambazo maji hayakatiki mara kwa mara na inapotokea mvua kubwa basi na mabonde kujaa maji inakuwa vigumu kwa mkulima huyu mdogo mdogo kuendelea na kilimo hichi.
    Na kama umefanya utafiti wa kutosha wakati mabonde yanakuwa yamejaa maji bei za mchichi zinapandaga sababu wakulima wanakuwa ni wachache sababu hii inafanya kudhibitika kwamba mboga nyingi zinalimwa sehemu maji yanatwama.Mkulima anayetaka kufanya kilimo hichi kibiashara basi anaweza tumia changamoto hii kama fursa kwake pia.
    •    NGUVU KAZI
    Nguvu kazi ni muhimu katika kilimo hichi sababu itaitajika kijana wakulima shamba na kuliandaa au kama shughuli zako hazikubani basi unaweza fanya mchakato huu mwenyewe ukaokoa gharama za za nguvu kazi.Lakini ukilinganisha na mauzo bado unauwezo wa kuajiri mtu kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza mradi huu chini ya usimamizi wako.
    •    MAUZO
    Mauzo ya mchicha kama utauzia shambani kwa bei ya tuta jumla kiwango cha chini ni 30,000 tumeweka kiwango cha chini ili ili kuweza pata kiasi halisi katika kadirio la chini.
    Kwa matuta 40 ukizidisha na bei ya chini ya tuta moja basi unakuwa umetengeneza 1,200,000/= yaani milioni na laki mbili shilingi za kitanzania.
    •    MUDA WA SUPERLISHE
    Ikumbukwe kwamba superlishe kupandwa mpaka kuanza kuvunwa basi inatumia karibia siku 21kwa hiyo kwa mahesabu ya kawaida kwa mwezi katika hekari moja unauwezo wa kutengeneza shilingi za kitanzania milioni moja na laki mbili.

    •    CHANGAMOTO
    Kufanya kilimo hichi kibiashara basi ni vyema kuhakikisha kwamba unazifahamu changamoto zinazoweza kukufanya usifikie malengo.Changamoto hizi ni kama:

    MAGONJWA:
    Mchicha wa super lishe unakubwaga na magonjwa kama ya kujisokota majani na kutobolewa majani dawa na kinga zake zipo kwenye maduka ya dawa za kilimo,pia ni vyema kuonana na maafisa kilimo kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu.

    MASOKO:
    Ni vyema kutafuta masoko ili kuweza kuwa na uhakika wa wateja wako kama utataka kutumia fursa hii kibiashara.Masoko ya mboga hii ni sehemu ambazo unaweza kubaliana kuingia mikataba kwa kupeleka mboga hii kwa makubaliano ya muda mrefu au mfupi.Sehemu hizi ni kama Mashuleni,Mahotelini,Migahawa ,Sokoni n.k
    Tunapenda kuwapatia fursa hii ambayo tunaona kwamba inaweza kuwa njia ya vyanzo vya mapato yako au njia ya kuongeza mapato yako.Unaweza endelea na utafiti kuweza fahamu mambo mengine ambayo tumeyagusia juu juu au hatukuyagusia kabisa.







    Source: Fursatz.com






    No comments:

    Post a Comment