• MAMBO YA KUJUA KABLA YA KUANZA KULIMA

    MAMBO YA KUJUA KABLA YA KUANZA KULIMA

     Katika ulimwengu wa sasa ushindani ni mkubwa sana,katika hili ni vyema kabisa kutambua kwamba biashara yoyote unayoifanya ni vyema kujiuliza mambo mengi na kufanya utafiti mzuri ili kuwa na njia dhabiti ya kukabiliana na changamoto zilizoko kwenye hiyo biashara husika au shughuli husika unayotaka kuifanya.

    RASILIMALI
    Ni vyema na sahihi kabisa kufanya tathmini ya rasilimali zilizoko kabla ya kufanya maamuzi sahihi ya nini kukipanda,swala hili litakusaidia kuangalia rasilimali ulizonazo zinawezesha kufanya kilimo gani,labda cha matunda au mbogamboga n.k.

    UTOFAUTI WA MAZAO
    Mazao kama matunda haya hutumia muda mrefu kuanza kuzaa.Kwa hiyo hutumia mtaji mkubwa kwa ajili ya kukuzia miti kabla haijazaa matunda.
    Mboga mboga nyingi hazitumii muda mrefu tokea kupandwa mpaka kuanza kuvunwa.
    Mazao mengine kama maindi,mchele,maharage n.k muda wake ni wawastani kulinganisha na baadhi ya matunda.
    Changamoto sio aina ya mazao bali ni kuwa makini katika uchaguzi wa zao husika,pia kutafakari kwa makini mwenendo wa soko katika zao ulilolichagua.

    MATATIZO YA ZAO HUSIKA
    Kama katika utafiti utagundua kwamba zao husika lina changamoto zake na kufahamu kwamba utatuzi wa changamoto hizo ni wa gharama zaidi, basi unaweza amua kubadili na kuelekeza nguvu kwenye zao jingine.Ila kama changamoto hizo zinatatulika basi ni unauwezo wa kuzikabili kwa kuendelea na zao hilo.

    SOKO LA MAZAO
    Kabla ya kuanza kulima mazao yako kibiashara ni lazma kufanya utafiti wa masoko yakoje.Yapo maswali yamsingi ambayo inabidi kujiuliza ili kujua soko lako vyema.Maswali hayo ni kama:
    1.    Wateja wako ni kina nani?(Hapa lazma uangalie kwa wakati uliopo na wakati wa badae),
    2.    Wateja wako wanahitaji nini?,
    3.    Wateja wako wataitaji hilo zao kwa kiasi gani?,
    4.    Wanahitaji nini na kwa wakati gani na ni wakati gani wakuuza?
    5.    Na je zao hilo wanaloitaji wateja wako wako tayari kulipa kiasi gani?
    6.    Lazma kujiuliza wateja unaowalenga wanatosha,au mbinu nyingine zitumike ili kuvuta wateja wengi au kiasi gani kizalishwe?
    7.    Namna gani unaweza fikisha mazao yako kwa wateja?

    USHINDANI KWENYE SOKO
    Katika biashara yoyote ni vyema kujua washindani wenzako kwenye biashara husika.Katika eneo hili yapo maswali mengi ya kujiuliza,mfano.
    1.    Nani mwingine analeta mazao kama yako kwenye soko au sehemu lengwa uliyokusudia?
    2.    Kuna mtu au kikundi cha watu flani kinachomiliki soko?
    3.    Bei za mazao husika zikoje (wakati wa msimu na wakati usio wa msimu)?
    4.    Ushindani ni wa ubora wa mazao,huduma au ni ukubwa wa bidhaa husika?
    Kwa utafiti ulioufanyika inatambulika kwamba ni vyema kufanya tafiti kabla ya kuanza kufanya kilimo chochote na ikiwezekana shauriana na wataalamu waliobobea kwenye zao husika ili kuweza kulima kwa faida na kuinua vipato.
    Tukizingatia kanuni hizi itatusaidia sana kulima kibiashara na mafanikio yanapopatikana ndipo ujasiri unapozidi kuongezeka,kwa kuweza kujaribu zaidi.




    Source: fursatz.com





    No comments:

    Post a Comment