KILIMO CHA KISASA CHA MAHINDI
“Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa
11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th
day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia
mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na
mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti
mwanzoni...."
KUANDAA SHAMBA, KUPANDA NA KUPALILIA
1. Kuandaa
Shamba, Kusafisha, Kulima/Kutifua
Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya
msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati
unaotakiwa.
Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa
mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima.
Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
i). Jembe la mkono - wengi wanatumia
ii). Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
iii). Power tillers
iv). Matrekta
Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la
kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na
kuufanya kuwa tifutifu (kufanya isiwe na mabonge makubwa, wala isiwe vumbi
vumbi). Hii husaidia:
i). Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi
ii). Udongo kuweza kuhifadhi maji
iii). Udongo kuwa na hewa inayohitajika na mimea
iv). Ukuaji mzuri wa mimea hivyo kuongeza mavuno
2. Kupanda
Mbegu Bora
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika
upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo
ni:
i). Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika
miaka mingi katika historia ya kilimo
ii). Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile
zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi
mawili - composite varieties na mbegu chotara (Hybrids).
Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa
unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya:
i). Mwinuko kutoka usawa wa bahari
ii). Kiasi cha mvua katika eneo husika
iii). Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Mbegu za mahindi
zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, Situka na zingine zote
zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251 na H 615.
Pia mbegu mpya
zilizotangawa na Kamati ya Taifa ya Mbegu mwaka huu ni
· WE4102 · WE4106 · WE4110 · WE4114 ·
WE4115 kutoka ARI ILONGA.
Jinsi Ya Kuweka Mbolea Za Kupandia
Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya
kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye
eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya
kupandia. Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu
Mazao na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea
na udongo huondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama kuna uhaba
wa unyevunyevu.
Viwango Vya Mbolea Za Kupandia
Kiwango cha mbolea za
kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni
sawasawa na kiasi cha aina mbambali za mbolea za kupandia kama inavyoonyeshwa
kwenye jedwali namba 1.
Jedwali na. 1: Kiasi cha
mbolea za kupandia kwa inayopendekezwa kwa eneo (hektari au ekari)
Aina ya mbolea za
kupandia
|
Idadi ya mifuko ya
kilo 50 kwa hektari
|
Idadi ya mifuko ya
kilo 50 kwa ekari
|
Viwango kwa kila shimo
|
DAP
|
2
|
1
|
Nusu kizibo cha soda
|
Minjingu fosfati
|
3
|
1½
|
Kizibo kimoja cha soda
|
Minjingu Mazao
|
4½
|
2
|
Kizibo kimoja na nusu cha soda
|
Muda wa kupanda
Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzonimwa mwezi wa 11
baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th
day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia
mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na
mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni.
Katika msimu huu utayarishaji wa shamba hufanyika mwezi wa pili mwanzoni.
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja
kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro
tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa
afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.
Kupanda kwa nafasi
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za
kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia
kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo.
Kwa mfano nafasi zifuatazo zinaweza kutumika katika upandaji wa mahindi:
Nafasi
|
Idadi ya mbegu kwa
kila shimo
|
Kiwango cha mbolea
kutumia kizibo cha chupa
|
90 sm X 30 sm
|
1
|
1
|
90 sm X 25 sm
|
1
|
1
|
90 sm X 50 sm
|
2
|
2
|
3. Kupalilia
Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota
ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na
mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu
na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno.
Magugu yaweza kuondolewa wa palizi
ya mkono (yaani) kung’olea (ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa
jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES) hasa 2-4D.
Mbolea za kukuzia
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa
lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa
kirutubisho cha naitrojeni. Mbolea maarufu za kukuzia katika soko la Tanzania
ni kama:
AIna ya mbolea
|
Kiwango cha
kirutubisho cha naitrojeni
|
Urea
|
46%
|
Calcium Ammonium
Nitrate (CAN)
|
23%
|
Sulphate of Ammonia
(SA)
|
21%
|
Urea inakirutubisho cha naitrojeni
(N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni
nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali
ya chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni
nusu kizibo cha soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa
muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa
ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba halina
magugu.
Pia wakulima hutumia mbolea za
kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous
fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya
wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa
mls 50-80 ktk lita 15 za maji. Mbolea za
kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za
kila shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja. Minjingu
Mazao (kg50/ekari = gramu 10kwa shimo) pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo
mkulima yko huru kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake.
Viwango Vya Mbolea Za
Kukuzia Vinavyoshauriwa
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni
kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali
namba 2. Mbolea inayotumika mara kwa mara ni Urea. Hata hivyo mbolea zingine
kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. CAN inaweza kutumika kama
kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium. Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia
inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne
baada ya kupanda.
Jedwali na. 2: Kiasi cha mbolea za kukuzia kwa
inayopendekezwa kwa eneo (hektari au ekari)
Aina ya mbolea za
kukuzia
|
Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa hektari
|
Idadi ya mifuko ya
kilo 50 kwa ekari
|
Viwango
|
Urea
|
2
|
1
|
Nusu kizibo cha soda
|
CAN
|
4½
|
2
|
Kizibo kimoja cha soda
|
SA*
|
3
|
1
|
Nusu kizibo cha soda
|
Mambo Muhimu Ya
Kuzingatia
Kuweka mbolea: Sehemu za nchi ambazo
muda wa kukua mahindi ni mrefu (zaidi ya miezi mitatu), ni vyema kuweka mbolea
za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi
mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.
Kupalilia: Katika kilimo cha
mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota
kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba
katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya
magugu katika shamba.
- Utafiti unaonyesha
kwamba, shamba la mahindi ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza mavuno kwa
asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu
bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na
mbinu nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno
yake.
KUDHIBITI MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MAHINDI
Magonjwa Yanayoshambulia Mahindi
i) Maize streak virus
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa,
kupanda mapema, kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua
‘vectors’ kama vile inzi weupe (white flies).
ii) Smut (Fugwe)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Helerat ukifuata maagizo
kamili.
iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi)
Dawa/Kudhibiti: Tumia mbegu zinazostahimili
kuoza.
Wadudu Na Wanyama Wanaoshambulia Mahindi
a) Viwavi Jeshi
Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia
mahindi kwa kula majaniyake pamoja na shina. Wadudu hawa
huangamizwa/kudhibitiwa kwa njia zifuatazo;-
- Kuondoa vichaka karibu na shamba
- Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
- Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate 1ml/1l
b) Funza wa Mabua (Maize Stalk
Borer).
- Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi.
- Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa.
- Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota.
Njia za kudhibiti zinazotumika
- Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde km vile maharagwe
- Kung’oa mahindi yaliyoshambuliwa
- Sumu za asili mwarobaini
- Sumu za viwandani km vile Karate. pia waweza tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili.
c) Cutworms (Vikata
Shina)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Dragnet FT na ufuate
maagizo kamili.
d) Wanyama waharibifu
Kudhibiti: Kuwatishia na kuwafukuza wanyama.
Ili mkulima aweze kupata
mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu
washambuliao mimea na njia zinginezo.
KUVUNA,
KUKAUSHA, KUSAFISHA NA KUHIFADIHI
Kuvuna
Mahindi yako tayari kuvuna wakati
kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka
vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani ya mhindi kutolewa.
Kukausha
Kama mahindi hayajakauka vizuri
hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango
kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze
yakiwekwa ghalani.
Ili kujua kama mahindi yamekauka
vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya soda iliyokauka na uongeze kiganja
kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi
ikikwama kando ya chupa, basi mahindi hayajakauka vizuri.
Kusafisha
Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa
na vilevile mahindi mabovu huondolewa.
Kuhifadhi
Mahindi huhifadhiwa ghalani baada ya
kuwekwa viatilifu vya kuzuia bungua wa mahindi Njia za kisasa za uhifadhi
hutumiwa kama vile matumiz ya ACTELLIC SUPER DUST katika uwiano wa 1kg kwa
gunia 5-10 za ujazo wa 100kg. Kiatilifu kingine ni actellic solution katika rate
ya 5mls katika gunia moja la kg 100.
Njia nyingine ya kienyeji katika
kuhifadhi mahindi ni kuweka juu ya ghala ambalo chini yake kuna jiko la kupikia
ambalo hutoa moshi unaotumika kufukuza na kuua wadudu.
Source:
mogriculture
No comments:
Post a Comment