• KILIMO KWA TEKNOLOJIA YA GREENHOUSE

    KILIMO KWA TEKNOLOJIA YA GREENHOUSE

     Katika makala hii tunawaletea fursa ya Greenhouse, katika kuiangalia fursa hii tutagusia maeneo yafuatayo:
    • Utangulizi,
    • Historia yake,
    • Faida zake,
    • Inchi zinazofanya vizuri kwenye kilimo cha greenhouse,
    • Aina zake,
    • Mazao yanayoweza limwa kwenye greenhouse,
    • Mtazamo kuhusu kilimo cha kwenye greenhouse kwa inchi zinazoendelea.
    • Hitimisho.



    UTANGULIZI
    Ukifatilia makala na vyanzo vingi vya tafiti greenhouse imekuwa ikipatiwa tafsiri ya majina tofauti kwamfano:
     Nyumba ya Kijani ,
     Banda kitalu n.k
    Vyovyote tutakavyoendelea kuiita teknolojia hii tunaamini cha muhimu ni kuelewa maana yake halisi.
    Greenhouse(Banda Kitalu):ni teknolojia ambayo imekuwepo duniani kwa sasa ambayo hutumika kwaajili ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo tunaamini yatasaidia mimea au mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea au mazao haya hupandwa kwenye banda,au nyumba maalumu.
    Teknologijia hii inatumika haswa kuikinga mimea isiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa.Mazingira haribifu haya ni kama:
    • Upepo mkali,
    • Baridi kali,
    • Mvua kubwa,
    • Mvua za mawe,
    • Mionzi mikali ya jua,
    • Joto kali,
    • Wadudu pamoja na magonjwa.
    Greenhouse inasaidia kuilinda mimea au mazao dhidi ya changamoto  zilizoziainishwa hapo juu.

    HISTORIA YAKE
    Zipo makala ambazo  zinaonesha kwamba fursa hii ya greenhouse ilivumbuliwa huko kwenye inchi zanye baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita.Inchi zilizokatika ukanda wa baridi, mazao yanayopendelea joto ilikuwa haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo.
    Changamoto hiyo ndiyo iliyopelekea uvumbuzi wa suluhisho la changamoto hiyo, yaani uvumbuzi wa greenhouse.Inchi hizo zilianza kutumia teknlojia hii maana greenhouse ilikuwa na uwezo wa kutunza joto, wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama vile mbogamboga(nyanya,hoho n.k)na matunda.
    Japokuwa teknolojia hii kwa inchi zilizoendelea imeanza zamani sana,bado kwa inchi zinazoendelea teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.
    KUMBUKA:Teknolojia hii inatumika kwenye inchi zenye joto pia,japo kuna utofauti kati yake na zile za inchi za ukanda wa baridi.

    FAIDA ZA GREENHOUSE
    • Mavuno yanakuwa mara kumi hadi kumi na mbili zaidi kilimo cha eneo la wazi,ikitegemewa sana na aina ya mazao yanayolimwa,aina ya greenhouse na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya green house.

    • Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka.

    • Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka,maana hamna haja ya kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.

    • Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi mno.Aina ya umwagiliaji unaotumika hapa ni umwagiliaji wa matone.

    BAADHI YA INCHI ZINAZOFANYA VIZURI KWENYE KILIMO CHA GREENHOUSE
    Makala na majarida mbalimbali yanaonesha baadhi ya inchi zinazofanya vizuri kwenye kilimo cha greenhouse.Lakini sisi tutawaeleza bila mtiririko maalumu.

    • Marekani inamaeneo karibia ya hekta 4000 za greenhouse ambazo vyanzo vingi vinaeleza kuwa ni kwaajili ya kilimo cha maua.Na kilimo hicho kimekuwa kikichangia katika mapato ya inchi husika.

    • Hispania zinakaribia kuwa na zaidi ya kekta 25,000 na Itali ni hekta 18,500 zimefungwa greenhouse kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama pilipili hoho,strawberry,matango,nyanya n.k

    • Zipo makala zinazoonesha Uholanzi imejiimarisha vyema sana katika maswala ya greenhouse.Yapo makampuni makubwa ya kiholanzi yaliyojiwekeza vyema ndani na nje ya inchi katika teknolojia hii ya greenhouse katika kilimo cha mazao mbalimbali kama maua,matunda,mbogamboga.

    • Israel pamoja na kuwa na eneo lao kubwa ni jangwa ni moja ya inchi zinazotumia kwa upana zaidi fursa hii ya greenhouse na ni kati ya wauzaji wakubwa wa maua(cut flowers) nje ya inchi yao.
    Zipo inchi nyingi ambazo wawekezaji wa ndani wakubwa au wadogo wameshawekeza katika fursa hii na wengine kuweza kuvuka wigo wa mipaka na kuwekeza hata inje ya inchi zao.Fursa hii imekuwa ikiwatajirisha situ wawekezaji bali pia watumiaji wa bidhaa au mazao yanayozalishwa kwenye teknolojia hii na pia imeweza kunufaisha inchi mbalimbali katika maswala ya mapato ya biashara husika na kuzalisha ajira pia kwa jamii ya eneo husika.

    AINA ZA GREENHOUSE
    Tumeweza kujifunza kuwa greenhouse hizi zimegawanyika katika makundi mbalimbali,lakini utofauti wa makundi haya unasababishwa na vigezo vifuatavyo:

    1. Aina ya greenhouse kwa kigezo cha umbile(shape),hapa zipo aina kadhaa za greenhouse mfano:
     Quonset Greenhouse
     Saw tooth type
     Even span type greenhouse
     Uneven span type greenhouse n.k

    2. Aina za greenhouse kwa kigezo cha matumizi:
     Greenhouse zinazoongeza joto (kwa maeneo ya baridi)
     Greenhouse zinazopunguza joto(kwa maeneo ya joto)

    3. Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake :
     Greenhouse za miti,
     Green house zinazotumia mabomba,
     Greenhouse zinazojengwa kwa chuma.

    4. Aina za greenhouse kwa kigezo cha zana za ufunikaji:
     Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za vioo(glass)-hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali,ili kutunza joto kwa muda mrefu.
     Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plastic(plastic film)

    5. Aina za greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa:
     Greenhouse za gharama kubwa (high cost greenhouse),zinaweza kuwa zaidi ya milioni 50,
     Greenhouse za gharama za kati(medium cost greenhouse),zinaweza kuwa kati ya milioni 20 mpaka 50,
     Greenhouse za gharama ndogo(low cost greenhouse),kuanzia milioni 20 kushuka chini.
    Tafiti zinaonesha kuwa watu wengi katika inchi znazoendelea wanatumia greenhouse za gharama ndogo yaani zinazodondokea katika kipengele cha milioni 20 kushuka chini.

    MAZAO YANAYOWEZWA LIMWA KWENYE GREENHOUSE
    Katika vipengele tajwa hapo juu tumeweza gusia baadhi ya mazao yanayolimwa kwenye teknolojia hii ya greenhouse.Katika inchi zinazoendelea ambamo na inchi yetu inaingia yapo mazao mengi ambayo yanaweza limwa kwenye greenhouse,mazao hayo ni kama:
    •  Nyanya,
    •  Pilipili hoho,
    •  Maua,
    •  Matango na mazao mengine mengi.
    MTAZAMO  KUHUSU KILIMO CHA KWENYE GREENHOUSE KWA INCHI ZINAZOENDELEA.
    Tunaimani kuwa fursa ya kilimo cha greenhouse kitasaidia sana kuondoa changamoto za umbali wa upatikanaji wa vyakula au mbogamboga na hivyo kupunguza gharama kutokana na uokoaji wa gharama za usafirishaji na uifadhi/utunzaji wa mazao husika.
    Kutokana na jamii nyingi katika inchi zinazoendelea kulima mazao kwa msimu,mtumiaji wa teknolojia hii ya greenhouse anaweza lima kwa lengo la kipindi ambacho msimu wa zao husika unapokuwa umekwisha hii inasababisha pindi mazao yanapopanda bei kwa kigezo cha upatikanaji na umbali wa usafirishaji,mkulima kwa njia ya greenhouse anaweza kushikilia soko kutokana eneo lake anapopatikana na kuweza kumpunguzia gharama za usafirishaji kwa wateja wakubwa na wadogo kumfata sehemu anapolimia.
    Teknolojia hii ikitumiwa kwa maarifa makubwa na hesabu madhubuti itachangia
    •  Kuzalisha ajira,
    •  Kuongeza uzalishaji wa mazao husika kwa kukidhi malengo ya mkulima,
    •  Kukuza vipato vya mkulima husika,
    •  Kuiongezea serikali mapato katika biashara husika.

    HITIMISHO
    Tunashauri ili kabla ya kuanza shughuli za kilimo cha teknolojia hii ni vyema kuwasiliana na wataalamu wanaotoa huduma hii walioko hapa inchini kwaajili ya kujadiliana na kupata ushauri wa kitaalamu ili kukidhi haja na dhamira ya uwekezaji wako.
    Tunaimani fursa hii ya kilimo hichi cha teknolojia ya greenhouse kitakusaidia kukupa mwanga katika kuona fursa zilizoko kwenye kilimo .






    Source: Fursatz.com

    No comments:

    Post a Comment