• JINSI YA KULIMA KILIMO CHA TANZAWIZI

    JINSI YA KULIMA KILIMO CHA TANZAWIZI
    Jinsi ya kulima zao la tangawizi kibiashara.Katika kuangalia fursa hii tutalenga mambo yafuatayo:
    •    Utangulizi
    •    Aina za tangawizi
    •    Hali ya hewa
    •    Udongo
    •    Upandaji
    •    Mgonjwa
    •    Uvunajwi
    •    Soko la Tangawizi
    •    Hitimisho


    UTANGULIZI
    Zao hili linajulikana kitaalamu kama Zingiber officinale, likiwa linajulikana sana kwa matumizi yake kama viungo katika vyakula.Zao hili limekuwa likilimwa sana inchini India,China,Nepal,Nigeria na Thailand.Inchi hizi zimekuwa zikitumia zao hili kwa matumizi ya ndani na hata kibiashara kwa usafirishaji wa nje kwenye masoko ya kimataifa.
    Kwa hapa inchini kwetu zao hili limekuwa likilimwa katika mikoa ya Tanga, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Mbeya na mikoa mingine kwa uchache.
    Umaarufu wa zao hili umetokana na wigo mkubwa katika matumizi yake.Matumizi yake ni pamoja na:
    •    Kutumiwa kama kiungo ili kuongeza ladha iliyokusudiwa kwenye chakula husika,
    •    Katika vinywaji mbalimbali katika kuongeza harufu kwa kiwango kilichokusudiwa kwa mujibu wa vipimo,
    •    Imekuwa ikitumiwa katika matengenezo ya mikate,biskuti,keki, nyama za kusaga n.k
    •    Vipo viwanda vimekuwa vikiitumia katika matengenezo ya dawa kwa ajili ya tiba mbalimbali.
    •    Pia zipo makala zinazoelezea tangawizi kutumika katika matengenezo ya vipodozi mbalimbali.
    Kwa uchache tu wa matumizi haya yanatoa picha uhitaji wa zao hili katika soko la ndani kwa sasa na siku zijazo.

    AINA ZA TANGAWIZI
    Wakulima wengi wanasema hawana uthibitisho wa jina la tangawizi zinazolimwa kwa hapa inchini ila zipo kati ya White Africa(Jamaica) na Cochin (flint) hizi huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.Ni vyema kuwasiliana na wataalamu katika wizara ya kilimo au taasisi na mashirika yakilimo yanayotambulika ili kuweza kupata ushauri sahihi wa aina ya tangawizi iliyobora kwa kulima ikiendana na udongo husika.

    HALI YA HEWA
    Zao hili hustawi sana kwenye maeneo yenye hali ya kitropiki wakulima na wataalamu wengi wanasema zao hili hustawi kwenye nyuzi joto kati ya 20 na 25.
     
    UDONGO
    Swala la udongo ni swala muhimu zaidi kwa zao lolote.Ni vyema kuhakikisha kwamba unawashirikisha wataalamu kwanza kuanzia kwenye zoezi zima la upimaji wa udongo ili kujua kwa majibu ya  kitaalamu kwamba eneo lako linawezesha zao hili kustawi.Makala nyingi na wakulima wanaonyesha zao hili linastawi zaidi kwenye udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.
     
    UPANDAJI
    Wakulima wengi hupanda zao hili kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri kisichopungua kimoja na mara nyingi wanasema huweza kukatwa katika urefu wa sentimeta 2.5 mapaka 5.Katika ukubwa hekta moja huweza kupandwa kiasi cha kilo 800 mpaka 1700 za tunguu.
    Pia nafasi inayotumika katika zoezi zima la upandaji ni (23-30)sentimeta kwa (15-23) sentimeta na kina cha urefu wa sentimeta (5-10) na maranyingi zoezi hili la upandaji hupandwa katika matuta.Katika kilimo cha zao hili wapo wanaopanda na jamii nyingine ya mazao kwa ajili ya kuweka kivuli.
     
    MAGONJWA
    Yapo magonjwa yanasoshambulia zao hili,magonjwa hayo ni kama madoa kwenye majani ya tangawizi yanayosababishwa na viini vya magonjwa vijulikanavyo kama Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
    Kuoza kwa tunguu la tangawizi kunapo sababishwa na viini viitwavyo Pithium spp.Pia ungonjwa wa miziz fundo husababishwa na Meloidegyne spp.
    Suluhisho ya magonjwa haya ni vyema kumshirikisha mtaalamu wa ili aweze kukupa tiba au kinga katika changamoto za magonjwa haya,ili kukusaidia kufanya kilimo chenye tija na manufaa kibiashara.
     
    UVUNAJI
    Baada ya tangawizi kupandwa zoezi la kuvunwa huwa tayari baada ya zao hili kuwa na umri wa miezi tisa mpaka kumi.Tangawizi inapofikia muda huu,huwa tayari kwa kuvunwa .Moja ya viashirio ni pale majani yanapokuwa yamegeuka rangi kuwa njano na kusinyaa.
    Katika zoezi la uvunaji zimegawanyika katika makundi mawili:
    •    Tangawizi zinazoitajika kwa kuifadhiwa kwenye kemikali,
    •    Kwa ajili ya kukausha au kusaga.
    Katika kundi la kwanza ambalo linalenga kwaajili ya kuifadhiwa kwenye kemikali,tangawizi hizi huvunwa kabla haijakomaa sana/kabisa.
    Na katika kundi la pili ambalo ni kwa lengo la kukausha au kusaga,Tangawizi huvunwa baada ya kukomaa na tangawizi hizi huwa na nyuzi  nyuzi na ni kali zaidi.
     
    SOKO LA TANGAWIZI
    Kutokana na muorodhesho wa matumizi ya zao hili katika kipengele cha utangulizi, tunakiri kuwa soko la zao hili litazidi kukuwa siku kwa siku.Uhakika wa soko la ndani ni mkubwa na wazalishaji hawatoshelezi uhitaji wa bidhaa hii.Kauli hii inatokana na kulinganisha kuwa watu wengi wamekuwa wakilima katika msimu mmoja na mara nyingi katika msimu huu,bei ya tangawizi huwa chini kiasi flani na msimu unapofika tangawizi kuadimika sokoni bei yake hupanda juu.
    Ni vyema wakulima kutumia mbinu za kiasasa kama kilimo cha umwagiliaji katika sehemu hizi au mbinu nyingine za kilimo ili kutosheleza kwanza soko la ndani hata kipindi ambacho wakulima wachache wanalima.
    Kwa upande wa mjasiriamali ni fursa mojawapo ya kuangalia jinsi gani atatumia kipindi amabacho tangawizi hazipatikani kwa wingi sokoni kulima kwa kutumia mbinu za kilimo za kiasasa au kuangalia mbinu za kuifadhi tangawizi isiharibike kwaajili ya kufanya biashara wakati zimeadimika sokoni.
    Tunaimani pale changamoto zinapozidi ndipo fursa zilipo basi wakulima na wajasiriamali watatitazama fursa hii kwa jicho la tatu ili kuona fursa nyingi zilizojificha katika fursa ya kilimo cha zao hili.

    HITIMISHO
    Tunaimani fursa hii itatoa mwanga kwa wasomaji wa fursa hizi na pia inaweza kukupa njia ya kuanzia katika kufanya tafiti zaidi juu ya zao hili kabla ya kuamua ni eneo gani katika fursa hii utaanza kuifanyia kazi.
    Kuanzia kwenye kuelimisha wakulima,kulima zao hili,kuhifadhi,kutumia katika shughuli za vyakula kama una migahawa au hoteli na katika viwanda zote ni fursa zilizojificha katika fursa hii ya zao la Tangawizi.
    Tunaimani fursa hii itakusaidia wewe ,ndugu ,jirani au jamaa zako.Tuelimike sote na tuelimishe na wenzetu katika fursa zinazotuzunguka.












    SOURCE :fursatz.com

    No comments:

    Post a Comment