• ATHARI ZA KIMAZINGIRA KATIKA ULAJI WA KUKU



    ATHARI ZA KIMAZINGIRA KATIKA ULAJI WA KUKU
    Kuna sababu mbalimbali zinazoathiri ulaji wa kuku, athari hizo zinaweza zikamfanya kuku ale sana au asile kabisa. Zifuatazo ni sababu za kimazingira zinazoathiri ulaji wa kuku:-

     
    1. JOTO
    Ulaji wa chakula hupungua kadri joto la mazingira linavyoongezeka, kwan kama tujuavyo zoezi la umeng'enyaji wa chakula huongeza joto la mwili, na joto la mwili halitakiwi kupanda wala kupungua, hivyo basi ubongo unamuamuru kuku asile ili kudhibiti joto la mwili lisipande.
    Angalizo ni kwamba mfugaji anatakiwa achunge hali ya joto la banda, kwan hata akizidisha balbu au banda likikosa hewa ya kutosha pia inaweza kusababisha joto la mazingira kuongezeka na kupelekea kuku kukosa hamu ya kula hali amabayo itawafanya kuku wadumae.

    2. BARIDI
    Kipindi cha baridi kuku wanakula sana kwa sababu ubongo unamuamuru kuku ale sana kwa kuwa umeng'enyaji unatakiwa uwe mara kwa mara ili kudhibiti joto la mwili lisishuke

    3. MHEMUKO (STRESS)
    Banda likiwa chafu, au lipo sehemu yenye kelele za mara kwa mara, au umeweka kuku wengi katika banda dogo itawasababishia kuku kupata stress hali ambayo itawafanya kuku wakose hamu ya kula

    4. UPATIKANAJI WA MAJI
    Maji yanakazi kubwa sana katika umeng'enywaji wa chakula (digestion process), kwa hiyo kuku ukiwabania maji na ulaji wao pia utapungua, kwani zoezi la umeng'enyaji chakula utakuwa unafanyika taratibu sana hali ambayo itawafanya kuku kukaa muda mrefu bila kuhitaji chakula

    5. MUUNDO WA VYOMBO VYA CHAKULA NA MAJI
    Muundo mbovu wa vyombo vya chakula na maji utasababisha chakula au maji kuchanganyika na vitu visivyofaa (feed or water contamination) kama vile kinyesi hali ambayo itapunguza ulaji wa kuku.
      




    SOURCE: brandpoultryfeed

    No comments:

    Post a Comment