CROPS
MADHARA YA KUACHA BANDA LA KUKU CHAFU
Katika ufugaji kitu kikubwa na
muhimu kuzingatia ni usafi, bila usafi hata uwe unawapatia chakula aina
gani kuku hawawezi kufanya vizuri. Yafuatayo ni madhara yapatikanayo kwa
kuacha banda chafu
1. MRUNDIKANO WA VIJIDUDU VYA MAGONJWA
Kama
tujuavyo banda likiwa chafu kunakuwa na mazalia ya vijidudu vya
magonjwa kama vile kuhara damu (coccidiosis), homa ya matumbo (typhoid)
na mafua, magonjwa ambayo yanaweza kusababisha vifo vingi katika banda
lako na kupelekea kupata hasara.
2. KUKU KUDUMAA NA KUPUNGUZA UTAGAJI
Kuku
wakiwa katika ugonjwa wowote dalili ya kwanza kabisa ni kupoteza hamu
ya kula hali ambayo inawapelekea kudumaa kwa kukosa lishe bora. Na kwa
upande wa kuku wa mayai huwa wanapunguza kutaga au kutotaga kabisa kwa
kukosa nguvu ya kuzalishia (production energy).
3. "STRESS " KWA MFUGAJI
Mfugaji
anaweza kupata mhemuko (stress) kutokana na kutibu mara kwa mara bila
mafanikio kwa magonjwa yaleyale kujirudia, na wingi wa vifo vitavyokuwa
vinatokea kila siku.
SOURCE: brandpoultryfeed
No comments:
Post a Comment