• MATATIZO YALETWAYO NA UPUNGUFU WA VITAMINI "D" MWILINI MWA KUKU

    MATATIZO YALETWAYO NA UPUNGUFU WA VITAMINI "D" MWILINI MWA KUKU




    VITAMINI D
    Husaidia madini aina ya calcium na phosphorous kuchukuliwa na mwili ili kuimarisha mifupa na kutengeneza ganda la yai la kuku. Jua husaidia mwili wa kuku kutengeneza vitamini D.

    Dalili za Upungufu wa Vitamini D Mwilini
    • Rickets: Mifupa huwa laini(soft), hupinda, magoti huvimba, na midomo huwa laini. Hii hutokana na madini aina ya calcium na phosphorous kutojengeka kwenye mifupa.
    • Maganda ya mayai huwa laini.
    • Kukua polepole.
    • Mayai hupungua.
    • Uanguaji hafifu wa mayai.




    SOURCE: brandpoultryfeed

    No comments:

    Post a Comment