SABABU ZA KUKU KUDONOANA AU KULA
MAYAI
Kuku hula mayai kwa sababu nyingi sana ambazo zingine za zote zinaweza kuzuilika,
1. Tabia yao tu- Hapa utakuta ndo uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai,
2. Kuto kupata chakula cha kutosha- Hii ni moja ya sababu kubwa kabisa inayo pelekea kuku kula mayai.
3. Kukosa madini joto- Hii inaweza kuwa ndo sababu kuu ya kwa nini kuku wanakula mayai, kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe, na jua kwamba kwenye yai kuku huwa anatafuta lile ganda la juu pekee sema anapo donoa na kulipasua yai hujukuta anakula na ute na kiini ila yeye lengo lake hasa ni ganda la juu
4. Kuku kutagia sehemu nyeupe sana yenye mwanga mkari hupelekea kuku kula mayai.
5. Mayai kukaa muda mrefu bila kukusanywa baada ya kutaga- Hapa ni kwamba mayai yanapo kaa muda bila kukusanywa na kama yapo sehemu ya wazi sana hupelekea kuku waanze kutest na some time kusangaa nini hiki cheupe? katika kushangaa ni kitu gani hiki cheupe cha mviringo hujikuta wanatest kudonoa na matokea yake ni kupasua yai.
6. Lishe mbaya
7. Nafasi ndogo
8. Vyombo havitoshi
9. Kukosa shughuli
12. Banda chafu (Manyoya)
12. Ukoo
NAMNA YA KUZUIA KUKU KUDONOANA AU KULA MAYAI
1. Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba.
2. Maji yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani.
3. Sehemu ya kutagia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai alilo taga.
4. Madini joto ni muhimu sana.
5. Kuku wenye tabia za kula mayai unaweza chinja au kuuza.
6. Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehem ulionayo.
7. Usizidishe mwanga.
8. Banda liwe safi.
9. Weka vyombo vya kutosha.
10. Wape lishe bora.
11. Wape kuku shughuli kwa kuwawekea bembea na sehemu ya uwazi kwa ajili ya mazoezi.
12. Kata midomo ya juu.
13.Epuka ukoo wenye tabia hizo.
ANGALIZO
Muda mwingine unaweza zania kuku wanakula mayai kumbe sio wao na wanasingiziwa tu, unaweza kuta ni vijana wa kazi/wafanya kazi wanakula au kwenda kuuza, paka, mbwa na hata nyoka so check out
SOURCE: brandpoultryfeed
No comments:
Post a Comment