• UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU (broilelers)

    UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU (broilelers)

    Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri
    a) Viinilisha vya wanga 60-65%
    b) Protini 30-35%
    c) Madini 2-8%
    Pamoja na maji safi yenye mchanganyiko wa dawa ya vitamin.
    Chakula cha vifaranga
    Chakula hiki utengenewza kati namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hutakiwa kuwa katika punje punje ndogo ndogo. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.
    Aina ya vyakula Kiasi (kgs)
    Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40
    Pumba za mtama au mahindi au uwele 27
    Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20
    Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25
    Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10
    Chumvi ya jikoni 0.5
    Virutubisho (Broiler premix) 0.25
    Total 100kgs.

    Chakula cha kukuzia – growers mash
    Aina ya vyakula Kiasi (kgs)
    Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25
    Pumba za mtama au mahindi au uwele 44
    Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17
    Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25
    Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 10
    Chumvi ya jikoni 0.25
    Virutubisho (Broiler premix) 0.5
    Total 100kgs.

    Chakula cha kumalizia kukuzia (Growers finisher
    s)
    Aina ya vyakula Kiasi (kgs)
    Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 31
    Pumba za mtama au mahindi au uwele 38
    Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 18
    Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25
    Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 13
    Chumvi ya jikoni 0.5
    Virutubisho (Broiler premix) 0.25
    Total 100kgs.

    No comments:

    Post a Comment