MASWALI MUHIMU YA KUJIULIZA KATIKA UFUGAJI WA KUKU
Kwanini tufuge kuku wa kienyeji?
Unapowauliza ni kwanini tufuge kuku wa kienyeji, wengi watakujibu kuwa hawapati maradhi mara kwa mara na hawana gharama kubwa za ufugaji. Lakini unapomuuliza mtu kuwa kuku wako alitotoa vifaranga 12 lakini mwisho mbona wamebakia wane, hatokuwa na jibu.
Kwa kawaida vifaranga hufa kwa maradhi ambayo wakati mwingine hutokana na kutowapa chanjo na wakati mwingine ni lishe duni.
Kweli kuku wa kitaalamu wanamatatizo?
Watu wengi wanadhani kuwa kuku wa kitalaamu wana matatizo wakati wa kuwafuga, lakini unapowauliza matatizo gani hayo, wengi wao hujibu kuwa wanahitaji gharama kubwa katika kuwatunza. Kitu ambacho si kweli kwa kuwa kila biashara inahitaji gharama. Kwa upande mwingine, wapo wafugaji si waaminifu hivyo husababisha baadhi ya watu kudhani kuwa kuku hawa hupewa dawa za binadama ili kuwa wakubwa.
Je, unaweza kufuga kuku bila gharama?
Kitu muhimu ni lazima tujue kwamba kitu chochote unachokifanya kwa biashara basi ni lazima ukifanye kitaalamu na kwa uweledi mkubwa. Kama unataka kufuga kuku lazima utimize masharti ya ufugaji bora ikiwamo kuwapa chanjo, chakula bora na dawa pindi wanapopata matatizo. Vitu vyote hivyo ni gharama.
No comments:
Post a Comment