• KILIMO BORA CHA BAMIA (OCRA)

    KILIMO BORA CHA BAMIA (OCRA)
    Bamia kwa lugha ya kigeni inaitwa Ocra ni aina ya zao ambalo hulimwa sana katika nchi za kitropiki pia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.Ni jamii ya zao la mbogamboga ambalo hutumiwa zaidi katika lishe.
    Bamia huwezwa kupikwa pamoja na nyama na likatumika katika lishe au hata kupikwa lenyewe peke yake na likatumika katika chakula.
    Zao hili huweza kulimwa kwenye ukubwa wa eneo lolote lile la ardhi.Huweza kulimwa kama zao la matumizi ya nyumbani au kulimwa kama zao la biashara kwa katika kiwango kikubwa.
    Zao hili humea kwenye maeneo yenye joto jingi hususan katika umbali wa mita 100 kutoka usawa wa bahari ni zao ambalo halivumilii baridi.
     

    Kiafya:
    Bamia ni aina ya zao ambalo lina wingi wa madini chokaa "calcium" ambayo husaidia zaidi katika kuijenga mifupa ya mwili na kwenye maeneo ya viungio halikadhalika kusaidia kunawirisha macho kuweza kuwa na nuru iliyo nnjema.
    Namna bora ya kupanda zao la bamia kibiashara zaidi ni kuzingatia kanuni za kilimo bora na chenye tija.Upandaji,ukuaji na hata uvunaji wa bamia ni lazima usimamiwe kwa ukaribu zaidi kwa ajili ya kuleta tija iliyokusudiwa.
     
    Ustawishaji:
    Zao hili hustawi katika mita 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.
     
    Kupanda:
    Kwa kawaida mbegu za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

    Tengeneza matuta ya urefu usiopungua futi1 chimba vishimo virefu na vichanganye na mbolea ya ng'ombe faida yake haiishi mapema kama ya kuku. Panda punje 2 kila shimo umbali wa hatua yako. Mwagilia maji asubuhi na jioni .Maji yawe yanatuama katika vishimo. Baada ya mwezi na nusu utaanza kuvuna bamia. Endapo maji ni ya kutosha basi kila ua la bamia likitoka utavuna bamia baada ya siku3. Likate na mkasi ili ukivuna usitoneshe mti wake kwa mavuno endelevu.Tena vuna makubwa madogo acha yakue. utaendelea kuvuna bamia kwa miezi isiopungua 2 kama mti
    inatunza vizuri.

    Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani.
    Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondoa ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka.
    Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

    Magonjwa:
    Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.
    Zao la bamia pia hushambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu ipuliziwe kwenye mimea ili kuweza kukua katika ustawi uliobora zaidi.
     
    Soko la bamia:
    Bamia ni zao ambalo lina soko nchi nzima na kila siku hutumika.
    Inakadiriwa kuwa ifikapo kipindi cha masika bei ya bamia sokoni huwa juu.Hivyo mkulima atakayekuwa na mavuno ya bamia wakati wa masika anatarajiwa kuuza kwa bei ya juu kwa kuwa kipindi hicho zao hili huwa adimu katika soko.Ukilima eneo lenye ukubwa wa ekari 3 faida yake huwa kubwa zaidi kwani debe kidogoo cha lita 10 huwa 5000-6000 fedha za kitanzania.Ukilima kipindi cha kiangazi ambapo zao hilo huwa jingi sokoni hukadiriwa kindoo cha lita 20 huuzwa 3000-4000 fedha za kitanzania.

    KWA MAONI NYONGEZA AMA USHAURI TUNAKARIBISHA MAWAZO YA WADAU WENGINE

    No comments:

    Post a Comment