• LIMA KILIMO BORA CHA MPUNGA SASA

    KILIMO BORA CHA MPUNGA
    Mpunga ni kati ya mazao ambayo yanalimwa sana dunian na pia ni kati ya mazao ambayo yanapendwa sana na watu kutokana na chakula chake juwa kitamu
    leo nitakupa muongozo wa jinsi ya kulima mpunga kitaalam  ili kuvuna mazao mengi yenye thaman
    siku zote maandalizi ya shamba vizuri ni jambo la msingi kwa kua bila kuandaa shamba lako vizuri huwezi kuvuna mazao yalio na ubora.
    Pia kunahatu za muhimu ambazo lazma mtu uzifate ili kufanyikiwa kupata

     
    1.KUSAFISHA SHAMBA
    Hii ni atu ya kwanza kabisa, unatakiwa kukusanya taka na mabaki ya mazao na kuyazika shambani ili kutengeneza mbolea aina ya mboji.,mara moja moja unaweza kukusanya taka na kuzichoma pale inapo itajika lakn kwa kua kuchoma huua wadudu rafiki.

    2. KULIMA
    Hii inaweza kufanya kwa kutumia jembe la mkono,trekta pamoja na jembe la ng'ombe.
    kulima inasaidia mbolea kuchanganyika vizuri, miziz kupita vizuri, hewa kupita vizuri katika ardhi pamoja na maji.
    unatakiwa kutifua 10-15cm na pia itasaidia magugu kuto ota mapema.

    3. KUTENGENEZA MAJARUBA
    Hapa unatakiwa kutengeneza kingo imara ili kusaidia maji kutopenya nje ya jaruba  na kingo inatakiwa kuwa ndefu kiasi ili kusaidia maji ya kutosha kuhifadhiwa ndani ya jaruba
     
    4. KUVURUGA
    katika kuvuruga unatakiwa kuweka maji 3-5 cm kutoka usawa wa bahari na kisha unavuruga ili kuweza kusababisha maji na udongo kuchanganyikana vizuri., hii inaweza kufanywa na jembe la mkono, trekta na jembe la ngo'mbe pia.


    5. KUSAWAZISHA SHAMBA
    Baada ya kuvuluga unatakiwa kusawazisha ili udongo uwe na kimo sawa na hii inaweza kufanywa na kutumia leki.
    hii usaidia katika upandaji pia kwa sababu aldhi inakua katika kimo kimoja.

    6. UPANDIKIZAJI MPUNGA
    Ili kupata mavuno mengi na kukifanya kilimo cha mpunga kuwa cha faida ni muhimu  wakulima kuzingatia mbinu hii muhimu na kuachana na kilimo cha kiholela kwa kumwaga mbegu moja kwa moja shambani. Aidha kwa wakulima wanaofuata kanuni hii wamepata mafanikio makubwa. 
    Faida zinazopatikana kwa kupandikiza mpunga
    •  Mkulima huweza kuchagua miche bora na mizuri ikiwa  kitaluni.

    •  Miche hukua haraka na yenye afya .
    •  Kiasi kidogo cha mbegu huhitajika.
    •  Mavuno huwa mengi.
    NJIA ZA KUPANDIKIZA MPUNGA
    •  Kupandikiza kwa mistari
    •  Kupandikiza bila ya kufuata mistari (Mchaka mchaka).
    Njia ya kupandikiza kwa msitari ndio njia bora zaid kwa kua inarahisisha katika  kupalilia pia inasaidia katika uvunaji napia utapata mazao mengi zaid kwa kua ulipanda kwa vipimo

      MAANDALIZI YA KUPANDIKIZA MICHE
    Kabla ya kupandikiza miche shambani ni muhimu kufanya maandalizi yafuatayo:  
    •  kumwagilia miche kwanza ili kupata urahisi wa kungo’a
    •  Ili kuzuia miche isikatike ovyo, miche ing’olewe kwa kushikwa chini zaidi ya shina
    •  Epuka kung’oa miche mingi kwa wakati mmoja
    •  Miche ifungwe kwenye mafungu madogo madogo ili kurahisisha usafirishaji na upandikizaji  shambani
    •  Miche bora tu ndio ichaguliwe. Sifa za miche bora
    •  Iwe na kimo kinacholingana, 
    •  Iwe na majani mafupi yaliyosimama, yenye mizizi mingi na yenye afya, isiyoshambuliwa na wadudu wala magonjwa, 
    JINSI YA KUPANDIKIZA MICHE
    •  Miche ishikwe  kwa vidole vitatu kama inavyoosha kweye picha chini 
    •  Pandikiza kati ya miche 2 -3 kwa kila shina
    •  Kwa mafanikio zaidi, miche ipandikizwe katika kina cha sentimita 2-3.
     NATUMAINI UMEJIFUNZA NA KUFAHAMU MENGI ZAIDI KUHUSU KILIMO CHA MPUNGA TUE PAMOJA TENA WAKATI MWINGINE
     
     
     
     
     
    SOURCE:Tanzanianakilimo 
     

    No comments:

    Post a Comment