• FAHAMU UGONJWA WA MAHEPE KWA KUKU ( MARECK'S DISEASE)

    MAHEPE (MARECK'S DISEASE)

    Huu ni ugonjwa unaowapata kuku, ambao unasababishwa na kirusi aina ya "HERPES VIRUS"

    Njia za Kuenea au Kusambaa kwa Ugonjwa

    • Kuchanganya mayai yenye ugonjwa na yasiyo na ugonjwa
    • Katika mashine za utotoleshaji vifaranga
    • Mayai ya kuku mwenye ugonjwa huu
    Dalili za Ugonjwa wa Mahepe (Mareck's Disease)
    • Kuvimba nerves


    • Miguu na mabawa kuishiwa nguvu (kupooza)
    • Kupungua uzito

    • Sehem ya kuifadhia chakula (crop) kutanuka

    • Macho huharibika na kuwa kipofu (jicho moja au yote)

    • Ngozi huumuka (kuwa nene)

    • Viungo vya ndani huwa na uvimbeuvimbe mweupe

    • Hukosa hamu ya kula

    • Kupooza viungo na vifo hutokea hasa wiki ya 10 hadi 20

    • Kuharisha

    Namna ya Kudhibiti na Kukinga
    Kuku wapewe chanjo wakiwa na umri wa siku moja (1)

    Tiba:
    Hakuna matibabu yaliyogundulika kisayansi, ila kama ugonjwa huu umeingia katika mifugo yako wasiliana na daktari au mtaalam wa mifugo aliye karibu yako.




    SOURCE: brandpoultryfeed

    1 comment:

    1. Mbona maelezo yenu huwa hayawezi kumfanya msomaji akaelewa kwa urahisi?hebu jitahidini mnapoweka masomo yenu yawe kwa upana kidogo kumfanya msomaji aekewe

      ReplyDelete